Jana
Jumatatu ilikuwa ni siku ya nomination katika big brother na majina
yaliyopata kura nyingi yaliongozwa na Feza wa Tanzania aliyeongoza kwa
kura 4 akifuatiwa na Bimp na Cleo waliopata kura 3 kila mmoja.
Kilichokuwa kinasubiriwa ni HOH kutumia nafasi yake ya kumuokoa
mshiriki mmoja aliyeingia katika nominations kwa kumuweka mwingine, na
mnigeria Beverly anayeiongoza nyumba wiki hii aliamua kumuokoa kipenzi
cha wengi kwa sasa Bimp na nafasi yake kumuweka mrembo Dillish.
Hivyo washiriki watatu ambao wako kikaangoni wiki hii ambao imetokea
kuwa wote ni wasichana ni Feza (Tanzania), Dillish (Namibia) pamoja na
Cleo (Zambia).
Je unadhani kuondoka kwa Bimp katika kikaango cha wiki hii kutasaidia
kuongeza kura za kumuokoa Feza kutokana na kuwa mshindani mkubwa Bimp
yuko salama? Kura yako inahitajika kumuokoa Feza anayeipeperusha bendera
ya Tanzania

إرسال تعليق