Chama cha wananchi CUF kimemuomba rais wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete kuchukua hatua juu ya vyombo vya dola
vinavyoendeleza tabia ya kutumia vyombo vya moto kukabiliana na raia na
kusababisha majeraha na hata kupelekea mauaji ya raia kwa kigezo cha
kulinda amani.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa chama hicho Profesa
Ibrahim Lipumba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu
tukio la kupigwa risasi kwa sheikh Ponda Issa Ponda huko mjini Morogoro .
Aidha Profesa Lipumba amesema amefanikiwa kwenda kumuona katika hospital
ya taifa Muhimbili na kusema amepigwa risasi bega la kulia
إرسال تعليق