BAADHI
ya watu kwenye jamii wamezoea kusikia au kuona wasanii kibao wakifanya
mambo ya ajabu na kuwa na skendo za hapa na pale kama kupigana, mapenzi
na kuzungumza mambo yasiyofaa lakini leo tunakuletea listi ya mastaa
wanaojiheshimu kwa hapa Bongo...
SALOME
NDUMBAGWE MISAYO ‘THEA’Ni staa wa kitambo wa filamu za Kibongo. Ni mke
wa ndoa wa mwigizaji Michael Sangu ‘Mike’. Thea amekuwa ni mfano wa
kuigwa na kila msanii anayetaka au anayeingia kwenye tasnia ya filamu na
jamii kwa jumla. Thea siyo mtu wa skendo kama walivyo wasanii wengine
wa kike Bongo.
Amedumu
kwenye sanaa kwa muda mrefu akianzia Kundi la Sanaa la Kaole wakati wa
michezo ya runingani leo, leo amefikia hatua ya kucheza filamu zake
mwenyewe japokuwa kumekuwa na malalamiko haonekani sana kama zamani.
SUZAN LEWIS ‘NATASHA’
Ni mkongwe wa maigizo ambaye ni mama wa mtoto mmoja. Natasha ni
msanii mwenye heshima tele kwenye tasnia ya filamu Bongo ambapo hivi
karibuni aliingia kwenye ndoa ya uzeeni kwani alikuwa hajaolewa hivyo
kuamua kutimiza agizo la Mungu alilowapa wanadamu.
Natasha hajawahi kuripotiwa na skendo yoyote kama baadhi ya wasanii walivyozoeleka kuwa kila siku ni watu wa matukio ya ajabu.
ILLUMINATHA POSHI ‘DOTNATA’
Dotnata ni staa wa maigizo, muziki na ni mjasiriamali. Ni mama
asiyekuwa na skendo na hivi sasa ameokoka na amekuwa akiwashauri wasanii
mbalimbali wabadilike lakini jitihada hizo zimekuwa zikigonga mwamba
kutokana na wengi wao kutosikiliza ushauri wake.
Wengine humsikiliza na kumwambia asubiri kwanza wamalize starehe zao.
WASTARA JUMA
Ni
mwigizaji ambaye ni mke wa aliyekuwa msanii wa filamu za Kibongo,
marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’. Wastara amekuwa ni mfano wa kuigwa na
wanawake wote ulimwenguni na siyo wa filamu pekee.
Wastara ni mchapakazi, hana muda wa
kukaa na kufanya mambo yasiyofaa kama kuendekeza wanaume, majungu na
kupigana kama ilivyo kwa wengine.
RIYAMA ALLY
Mwanadada wa filamu za Kibongo anajiheshimu na amejaliwa kuwa na
mtoto mmoja wa kike. Hajawahi kuripotiwa na skendo. Mara nyingi yupo
bize na kazi zake na huwezi kukutana naye kwenye kumbi za starehe usiku
au katika makundi yasiyofaa.
Kwenye filamu Riyama anakubalika kutokana na uigizaji wake wa kiuhalisia zaidi.
YVONE-CHERRY NGATIKWA ‘MONALISA’
Huyu ni mtoto
wa Natasha ambaye kafuata nyayo za mama yake katika tasnia ya filamu
Bongo. Monalisa ni mama wa watoto wawili.
Hana skendo na anajiheshimu na
kujielewa yeye ni nani katika jamii
Post a Comment