
Wakati Henry amerejea kwa mara nyingine Simba baada ya kumaliza mkataba wa kuichezea Kongsvinger ya Norway mwezi uliopita, Kaze na Tambwe ambao itakuwa ni mara yao ya kwanza kuonekana kwa mashabiki wa jijini Dar es Salaam kwani hawakuwepo katika tamasha la maadhimisho ya klabu hiyo 'Simba Day' ambalo liliambatana na utambulisho wa wachezaji na jezi mpya.
Katibu Mkuu wa Simba Evodius Mtawala, amesema kuwa maandalizi ya mchezo huo yanakwenda vema na kwamba kikosi cha Simba kilichokuwa Arusha kwa mchezo wakew wa Ligi kuu bara dhidi ya JKT Oljoro kinatarajiwa kurejea jijini kesho.
"Nawaomba mashabiki wa Simba wajitokeze kwa wingi siku hiyo kuwashuhudia wacvhezaji wetu wapya,"alisema
Ikumbukwe kuwa Henry alijiunga na Kongsvinger mwaka 2009 akitokea klabu ya Simba.
إرسال تعليق