Hii ndio movie mpya iliyomtoa machozi Raisi Obama

Raisi wa marekani Barack Obama amesema katika interview iliyoruka siku ya jumanne kuwa alitokwa na machozi wakati alipokuwa akiangalia movie mpya ya  Lee Daniels "The Butler", Movie inayomhusu mtumishi mweusi (White house) ambae alifanya kazi kwa maraisi 7 kadhaa.

nilitokwa na machozi nikifikiria sio tu kuhusu mtumishi aliekuwa akifanya kazi hapa ikulu, lakini kizazi chote cha watu ambao walikuwa wenye vipaji na wenye ujuzi Lakini kwa sababu ya Jim Crow na kwa sababu ya ubaguzi., hawakuweza kufika mbali ," Rais alimwambia mtangazaji wa redio "Tom Joyner", katika interbiew hiyo iliyofanyika Ikulu.



 "Na bado kwa hadhi na mshikamano, Wakaamka na kufanya kazi kila siku na kukabiliana na kila aina ya fujo kwa sababu walitumaini mazuri kwa ajili ya watoto wao." aliongezea Obama

Raisi Obama pia amesema sehem iliyomfurahisha katika movie hiyo ni wakati muigizaji Cuba Gooding Jr alipokuwa akitoa vichekesho lakini alisisitiza ni vichekesho ambavyo maneno yake hawezi kuyarudia redioni, pia amewasifia sana waigizaji Forest Whitaker pamoja na Oprah Winfrey.

"I thought Forest Whitaker was wonderful," Obama said. "And Oprah, my girl, she can act. She's just a wonderful actress, so I'm glad they did it." amesema Obama

Post a Comment

Previous Post Next Post