Jana
50 Cent aliingia mahakamani kwa mara ya kwanza ambapo wakili wake
alidai hana hatia katika kesi inayomkabili ya kumpiga mchumba wake wa
zamani na mama wa mwanae. Madai mengine ni pamoja na kuharibu mali.
50 ambaye jina lake halisi ni Curtis Jackson, aliambiwa kukaa mbali
na mchumba wake huyo wa zamani Daphne Narvarez na alikatazwa kuwasiliana
naye kwa simu ama email. Aliambiwa pia hatakiwi kumiliki silaha na
aliambiwa kurejea tena mahakamani Sept. 4.
Narvarez anasema 50 alimshambulia kwenye nyumba yake ya California na
kumpiga huku polisi wakisema aliharibu mali yenye thamani ya $7,100.
Post a Comment