Hivi ndivyo 50 Cent alivyokana mashtaka ya kumpiga ex wake

50cent_070313Jana 50 Cent aliingia mahakamani kwa mara ya kwanza ambapo wakili wake alidai hana hatia katika kesi inayomkabili ya kumpiga mchumba wake wa zamani na mama wa mwanae. Madai mengine ni pamoja na kuharibu mali.
50 ambaye jina lake halisi ni Curtis Jackson, aliambiwa kukaa mbali na mchumba wake huyo wa zamani Daphne Narvarez na alikatazwa kuwasiliana naye kwa simu ama email. Aliambiwa pia hatakiwi kumiliki silaha na aliambiwa kurejea tena mahakamani Sept. 4.
Narvarez anasema 50 alimshambulia kwenye nyumba yake ya California na kumpiga huku polisi wakisema aliharibu mali yenye thamani ya $7,100.

Post a Comment

أحدث أقدم