Imeandikwa na Baba wa Taifa
Hivi karibuni kumezuka mtindo wa wizara ya fedha au wizara yenye
mamlaka ya wafanyakazi wa serikali kufanya uhakiki wa wafanyakazi wao.
Kinachoangaliwa ni:
Kiwango cha elimu kama ni sahihi au kama hawakughushi vyeti; umri wao
mnasaba na vyeti vyao vya kuzaliwa (wengine wameghushi umri ili
kuongeza muda wa kufanya kazi serikalini zaidi na zaidi); mishahara yao –
wengine mishahara wanayopokea hailingani na elimu zao: diploma atalipwa
mshara wa digrii, na wa digrii analipwa wa cheti inategemea umeegemea
wapi kisiasa au ukaribu wako na watendaji wakuu wa wizara.
Mfano mzuri tu ni wizara ya elimu. hii imeoza kwa mishahara hewa na
wafanyakazi hewa. Kimantiki, haiwezekani kuwa na mfanyakazi hewa au
mishahara hewa bila watendaji wa wizara kuhusika. Haiwezekani aslan
abadan.
Zoezi hili la kuhakiki wafanyakazi wa serikali limefurutu ada has
mwezi huu wa Ramadhan. Walimu wanakwenda kupiga magoti katika vituo
mbali mbali kwa madai kuwa wanasubiri kuhakikiwa au kusubiri mishahara
yao.
Juzi tu, walimu wa Kiembe Samaki walikaa mpaka saa tatu usiku eti
wanasubiri watoaji wa mishahara na kuhakikiwa. Baadhi yao tumewauliza
‘mmefutari wapi’ je, hao waliokuiteni wao ni waislamu (wanafunga au
hawafungi). Hizi ni adhabu ambazo si za lazima kwa watendaji wa
serikali, ni ubovu wa watendaji wetu wa serikali, wanaonekana kuwa sio
mahiri wa kumudu kazi zao walizopangiwa.
Hivi kila siku wafanyakazi hawa wanahakikiwa lakini uoza unabaki pale
pale. Isitoshe, hawa watendaji wa wizara ya elimu hawana record za
nyuma, maana umemhakiki mwalimu, mwezi wa februari, halafu, mwezi wa
Juni, baadaye julai, na unauliza maswali hayo hayo kila siku, ukiuliza
wanakwambia ‘computer zetu imeharibika’ au hawana kabisa kumbukumbu.
Hapa ipo namna. Ama watendaji wa wizara husika wana mpango na wao
kufanya ‘magube magube’ au ni sehemu ya mtandao wa huo wizi unaofanyika
na ghilba za wafanya kazi hewa.
Hivi kwa nini hatujasikia hata mwalimu mmoja au mtendaji wa wizara
husika amefukuzwa kazi au ameadabishwa kw akosa kama hili, ilhali
wanajulikana?
Tukumbuke kuwa athari ya zoezi hili lisilokwisha ni mambo mengi:_
Sheikh AHMEID — hapa jaza wewe, then uirushe (jina langu baba wa Taifa)
– Ahsante–
Baba wa Taifa
Baba wa Taifa
Wengi wa walimu hawa wanachukua mishahara yao benki, na sasa benki hiyo PBZ imekosa biashara
إرسال تعليق