HABARI
zilizochimbuliwa kwa undani zinadai kuwa tayari vigogo wawili waishio
nchini wamebanwa na Jeshi la Polisi Tanzania wakituhumiwa kumtuma
Masogange kupeleka madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini.
Agnes
Gerald 'Masogange' Kwa mujibu wa habari hizo, vigogo hao (majina
tunayo) walidakwa wiki iliyopita kila mmoja kwa wakati wake na kuhojiwa
katika Kituo Kikuu cha Polisi (Central), jijini Dar ambako walihojiwa
kwa saa sita.
“Hawa vigogo
walikamatwa wiki iliyopita na kuhojiwa kwa masaa sita, waliachiwa lakini
waliambiwa wakihitajika tena wataitwa,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo kikaongeza kuwa, licha ya kuhojiwa na kuruhusiwa kuondoka, vigogo
hao, mmoja alinyang’anywa ‘paspoti’ yake huku mwingine akaunti zake za
benki zikifungwa kwa muda usiojulikana.
Habari zinasema kuwa, kigogo
ambaye akaunti zake zimefungwa amekuwa akihaha kila kukicha kuhakikisha
zinafunguliwa kwa sababu hana njia nyingine ya kuingiza kipato.
Juzi, Ijumaa liliwasiliana na Kamanda wa Kikosi Maalum cha Kupambana na
Madawa ya Kulevya, Godfrey Nzowa ili kujua uhakika wa madai hayo ambapo
alisema:
“Sisi (polisi) tumekuwa tukifanya mambo yetu kwa siri
kubwa, si rahisi kusema. Tukisema kunakuwa na ugumu kwa sababu mnaandika
kwenye magazeti, matokeo yake uchunguzi unavurugika.
“Mfano wale
wasichana (akina Masogange) waliokamatwa Afrika Kusini wamekuwa wagumu
kuwataja waliowatuma kwa sababu hao waliowatuma ndiyo wanaowategemea
kuwawekea dhamana.”
Agnes Gerald na mwenzake, Melisa Edward
walikamatwa Julai 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Oliver Tambo uliopo Kempton Park nchini humo wakiwa na madawa ya kulevya
aina ya Crystal Methamphetamine yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.
إرسال تعليق