Baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni ya Serengeti Breweries wakionesha muonekano mpya wa chupa ya Kibo Gold.
Meneja Miradi endelevu na uwajibikaji
lampuni ya bia ya Serengeti Nandi Mwiyombela (Katikati), Meneja wa mauzo
wa kanda ya kaskazini Patrick Kisaka (kushoto) na Attu Mynah (kulia) kutoka
idara ya mipango wakionyesha mbele ya wasambazaji
wa bia na waandishi wa habari aina mpya ya chupa yenye shingo ndefu ambayo bia
ya Kibo Gold itapatikana kuanzia sasa, hafla hiyo ilifanyika katika kiwanda cha
Serengeti Breweries kilichopo mjini Moshi.
Meneja
wa miradi endelevu na uwajibikaji Bi Nandi Mwiyombella akizungumza
jambo mbele ya Wanahabari na wageni waalikwa kwenye hafla ya muonekano
mpya wa bia ya Kibo Gold
Meneja
wa kiwanda cha bia cha Serengeti cha njinpi Moshi Bw. Coleman Hanna (katikati)
akibadilishana mawazo na meneja mauzo wa kanda ya kaskazini Bw. Patrick Kisaka
(kulia) wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa bia ya Kibo Gold uliofanyika
kiwandani hapo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Msambazaji
wa kwanza kabisa wa bia za Serengeti mkoa wa Kilimanjaro Mama Kisela, akipokea
bia ya Kibo Gold yenye muonekano mpya na ladha ileile kutoka kwa Attu Mynah wakati wa uzinduzi wa
muonekano mpya wa chupa wa bia hiyo katika hafla fupi iliyofanyika katika
kiwanda hicho wmwishoni mwa wiki.
========= ====== =====
KAMPUNI YA BIA YA
SERENGETI YAFANYA UZINDUZI WA MUONEKANO MPYA WA BIA YA KIBO.
*Sasa Kibo yang’ara katika chupa ya kisasa kabisa*
Kampuni ya bia ya Serengeti leo imezindua muonekano mpya wa bia inayosherehekewa sana
mkoani hapa, Kibo Gold. Uzinduzi huu uliofanyika katika kiwanda cha
bia cha Serengeti kilichopo Moshi, ulifikia kileleni kwa shughuli murua
iliyoandaliwa na kampuni hii na kushuhudiwa na waandishi wa habari pamoja na
wadau mbali mbali. Bia hii ya Kibo
sasa ina muonekano mpya wa chupa inayoashiria ubora wa kilichopo ndani. Bia ni yenye ubora uleule wenye kiwango cha
hali ya juu ila kwa chupa ya rangi ile ile iliyongarishwa na shingo ndefu.
Akiongea kwenye hafla hii Meneja wa miradi endelevu na uwajibikaji Bi Nandi
Mwiyombella alisema bia hii ya Kibo Gold imekuwa ikitambulika kwa ubora na ladha
nzuri kwa wateja. “Kwa muonekano huu
mpya wa chupa ya kisasa, tunaamini wateja wengi watavutiwa na kuipenda zaidi
kwani ni muonekano unaokwenda na wakati. Ubora wa bia hii, unakuwa dhahiri kweli
kabisa ukizingatia kwamba inatengenezwa kwa maji yatiririkayo kutoka katika
kilele cha juu kabisa cha mlima Kilimanjaro ambapo pia bia inazoa jina lake
hili la ‘KIBO’, aliongeza Bi Nandi.
Kampuni ya bia Serengeti
chini ya kampuni mama ya Diageo, inazingatia kanuni na sheria zilizowekwa na kampuni hii kwenye
ubora katika uzalishaji wa bidhaa
zote. Muonekano wa bidhaa ni ule
unaondena na soko za kimataifa na wa kuvutia.
Kampuni ya bia ya Serengeti
inatumia malighafi za kitanzania ili kuleta ubora halisi na vile vile
kukuza uchumi wa Tanzania katika sekta ya kilimo.
Kwa Mhariri: Bia ya Kibo Gold
ilirudishwa sokoni hapa Tanzania mwaka jana, 2012, mwezi wa sita baada ya kuwa
haipo kwenye soko kadri ya miaka kumi. Ni
mojawapo ya bia zinazoongoza nyanda za kaskazini sasa hivi. Bia hii inazalishwa katika kiwanda cha bia
cha Serengeti cha Moshi na inasambazwa mkoani hapo na mikoa jirani, Arusha,
Tanga, Manyara na Tanga kwa wingi.
Tafadhali
kunywa kistaarabu. Haiuzwi kwa walio
chini ya miaka 18.
Post a Comment