JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA
MALIASILI NA UTALI
TAARIFA KWA UMMA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
IMEKANUSHA UVUMI KUWA WATEULE WA WAZIRI WAMESAINI POSHO MBILI.
Wizara ya Maliasili na Utalii
inakanusha uvumi ulioandikwa na kuchapishwa na gazeti la Raia Mwema mnamo tarehe
07/08/2013 ukurasa wa kwanza lililobeba kichwa cha habari UFISADI kama wabunge, wateule wa waziri wasaini posho mara
mbili ikiwa na ufafanuzi kuwa yumo
Ofisa Takukuru,walipwa na taaasisi wanayoichunguza. Taarifa hii ilikuwa na
muendelezo zaidi ukurasa wa tatu wa gazeti hilo.
Wizara inasisitiza kuwa
uvumi huo siyo kweli kutokana na sababu zifuatazo:
·
Wajumbe
wa kamati husika (iliyoundwa kuchunguza tuhuma kuhusu matumizi mabaya ya fedha
unaowahusisha watendaji wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro) (NCAA) HAWAKULIPWA
POSHO MARA MBILI.
·
Malipo
waliyolipwa wajumbe wa kamati husika yalilipwa na Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro (NCAA) kama ilivyo kwenye Hadidu
za Rejea za kazi husika na hawakulipwa malipo yoyote na wizara ya maliasili na
utalii.
·
Viwango
vya posho vilivyotumika ni kwa mujibu wa Waraka wa Serikali namba 2 wa Mwaka
2010, Ref.Na C/AC/.17/45/01/125
·
Malipo
yaliyofanywa kwa wajumbe wa kamati husika yalikuwa na kibali halali cha Waziri wa
Maliasili na Utalii Mhe. Khamis Suedi Kagasheki
·
Kamati husika ilifanya
kazi vizuri na kukabidhi ripoti ya awali iliyomridhisha Waziri Kagasheki
aliyewaagiza kuifanya kazi tajwa hapo juu. Ripoti hiyo ya awali na hii ya
mwisho ZITAWEKWA HADHARANI ili Umma uelewe hali halisi ya Mamlaka ya Ngorongoro
na siyo upotoshaji wa Raia Mwema.
·
Kamati iliyoundwa na
Waziri Kagasheki ilikuwa na kazi tofauti na ile kamati ya awali iliyowahi
kuongozwa na Jaji Robert Mihayo aliyeteuliwa na aliyekuwa Waziri wa Maliasili
na Utalii, Ezekiel Maige mwaka 2011. Raia Mwema ingejiridhisha kwa kutazama
hadudi za rejea za Kamati hizo mbili. Si jambo jema Raia Mwema kuupotosha Umma.
Wizara ya Maliasili na Utalii
imesikitishwa na kitendo cha gazeti la Raia Mwema, gazeti ambalo limejijengea
sifa na kuaminiwa na jamii kwa kutoa
taarifa za uhakika zinazofuata maadili
ya utoaji taarifa kwa vyombo vya habari, kuchapisha habari zinazochafua jina la
Wizara, Wabunge na Serikali kiujumla bila kujihakikishia ukweli wa taarifa hizo
kutoka wizara husika.
Kwa taarifa hii, Wizara inalitaka Gazeti
la Raia Mwema kufuta uvumi waliochapisha kwenye gazeti lao kama ilivyotajwa
hapo juu na pia kuiomba radhi Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuchapisha
habari ambazo si sahihi na pia kuchafua jina la Wizara.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
12/08/2013
Post a Comment