Tume moja nchini Afrika Kusini
inayochunguza kashfa ya ufisadi ya mkataba wa mabilioni ya dola wa
silaha imeanza vikao vyake baada ya kuchelewa kwa miezi mitano.
Madai ya rushwa yameikumba serikali ya rais Jacob Zuma na pia iliyokuwa serikali ya Thabo Mbeki.Zuma pia alishtakiwa lakini kesi dhidi yake ilitupiliwa mbali kabla ya yeye kuingia mamlakani.
Wafuasi wake wamekuwa wakisisitiza kuwa alikuwa mwathiriwa wa kampeni chafu ya kisiasa.
Bwana Mbeki ni mmoja wa wanaotarajiwa kufika mbele ya tume hiyo kama shahidi.
Mkataba huo unasemekana kuwa mkubwa zaidi wa kifedha kuwahi kufikiwa baada ya enzi ya ubaguzi wa rangi , na lengo lake ilikuwa ni kuimarisha hadhi ya idara ya ulinzi.
Ilihusisha kampuni kutoka Ujerumani, Italy, Sweden,Uingereza, Ufaransa na Afrika Kusini.
Lakini madai ya ufisadi yalianza kuzingira kashfa hiyo.
Shaik alifungwa jela miaka 15 mwaka 2005 kwa kuitaka kampuni ya Thint, kumlipa kiasi fulani cha pesa.
Afisaa mwingine, Tony Yengeni, aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya ulinzi bungeni wakati mkataba huo ulipoafikiwa pamoja na kuwa kiranja wa chama cha ANC, alifungwa jela mwaka 2003 kwa kosa la ufisadi.
Hata hivyo aliachiliwa huru baada ya kuhudumia kifungo kwa miezi mitano licha ya kuwa alifungwa jela miaka minne.
Post a Comment