Jitihada za kimataifa za kutaka
kutatua mzozo wa kisiasa nchini Misri zinaendelea hii leo huku maseneta
wa marekani John Mc Cain na mwenzake Lindsay Graham wakitarajiwa
kuwasili mjini Cairo.
Mwishoni mwa juma ,naibu waziri wa maswala ya
kigeni nchini marekani William Burns aliongeza muda wa ziara yake nchini
humo ambapo amefanya mazungumzo na mkuu wa jeshi jenerali Abdel Fattah
al Sisi pamoja na waziri mkuu Hazem Beblawi mbali na wajumbe wa vuguvugu
la Muslim Brotherhood.Maafisa hao wawili kutoka marekani watakuwa nchini Misri katika ziara ya siku mbili kufuatia ziara nyengine ya naibu waziri wa maswala ya kigeni nchini marekani William Burns.
wakati wa ziara yake Burns alikutana na mawaziri kadhaa kutoka serikali ya mpito pamoja na viongozi wakuu wa vuguvugu la Muslim Brotherhood.-akiwemo Khairat al Shater ambaye amewekwa kizuizini akingojea kushtakiwa kwa kuchoche ghasia.
Huku wajumbe wa mataifa ya kigeni wakiimarisha juhudi za kusitisha umwagikaji wa damu zaidi nchini humo ,mamlaka ya taifa hilo inazidi kuwasihi waandamanaji wanaotaka kurejeshwa mamlakani kwa Mohammed Morsi kusitisha maandamano yao na kuondoka katika maeneo walikokita kambi.
Ndege ya serikali tayari imemwaga vijikaratasi kando ya msikiti mmoja Mashairiki mwa Cairo vyenye ujumbe wa kuwataka raia kuondoka eneo hilo kwa amani.
- Bbc
Post a Comment