Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Kiislam ya
IRAN Mhe. Al-Akbar Hashemi Rafsanjani wakati Makamu wa Rais alipofika
kwenye Makazi ya Rais huyo mjini Teheran Iran leo Ogast 05-2013, Makamu
wa Rais yupo Nchini Iran kwa ajili ya kuhudhuria kuapishwa Rais Mpya wa
Nchi hiyo alieapishwa jana jioni.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Kiislam ya IRAN Mhe. Al-Akbar
Hashemi Rafsanjani wakati Makamu wa Rais alipofika kwenye Makazi ya
Rais huyo mjini Teheran Iran leo August 05-2013, Makamu wa Rais yupo
Nchini Iran kwa ajili ya kuhudhuria kuapishwa Rais Mpya wa Nchi hiyo
aliyeapishwa jana jioni.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal,
kipata maelezo kutoka kwa maafisa wa Rais mstaafu wa Jamhuri ya kiislam
ya Iran alipotembelea makazi ya Rais Al-Akbar Hashemi Rafsanjani mjini
Teherani Iran leo Ogast 05-2013.(Picha na OMR Teheran).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
jana alikuwa mmojawapo wa wageni mashuhuri katika sherehe za kumuapisha
Rais wa mpya wa Jamhuri ya Kiislamu ya Watu wa Iran Mheshimiwa Hassan
Rouhani, sherehe iliyofanyika katika makao makuu ya nchi hiyo yaliyopo
jijini Tehran. Kabla ya sherehe hiyo ya kuapishwa, Jumamosi Agosti 4,
2013, Mkuu wa Kidini wa nchi hiyo Ayatollah Ali Khamenei alimthibitisha
Rais Rouhani na akatumia nafasi hiyo kufafanua kuhusu aina ya mahusianio
ambayo Iran inataka kuyaona baina yake na nchi zingine duniani.
Mheshimiwa
Makamu wa Rais alikuwa miongoni mwa viongozi wapatao 55 kutoka nchi
mbalimbali walioshiriki sherehe hizi huku vyombo vya habari kutokana
nchini Iran vikielezea kuwa tukio la jana kwamba ni la kihistoria kwani
Iran haikuwahi kuwa na wageni mashuhuri wengi kiasi hicho katika sherehe
zake za kuapisha viongozi wa nchi hiyo. Sherehe hizo pia zilihudhuriwa
na Rais aliyemaliza muda wake, Rais Mahmoud Ahmadinejad.
Akihutubia
wananchi wa Iran sambamba na wafutiliaji wa siasa za Iran mara tu baada
ya kuapishwa, Rais Rouhani alisema Iran inategemea kuwa nchi za
ulimwengu wa kwanza zitatafuta suluhu nayo kwa mazungumzo na siyo kwa
kutumia vikwazo. Kauli hii alikuwa anaitoa siku moja baada ya seneti ya
Marekani kupitisha kwa azimio moja vikwazo zaidi kwa Iran saa chache
kabla ya Rais Rouhani kuthibitishwa na Ayatollah Khamenei, Kiongozi
mkubwa kabisa na mwenye heshima ya juu katika Iran.
Wachambuzi
wa masuala ya kisiasa na kimashirikiano wanaamini kuwa serikali ya Rais
Rouhani ambayo aliitangaza mara tu baada ya kuapishwa, itaanza kazi kwa
wakati huku ikibadili uelekeo kutoka katika siasa za mrengo wa kushoto
na kuwa siasa za kawaida ambazo zitafungua mahusiano zaidi na nchi za
Mashariki.
Tanzania
ina uhusiano wa siku nyingi na Iran na siku kadhaa za mwisho wa utawala
wa Rais Ahmadinajad, Iran ilikubali kuifutia Tanzania deni lake
lililokuwepo kwa miaka mingi kwa lengo la kuimarisha mahusiano baina ya
nchi hizi mbili. Pia, Iran imekuwa ikisisitiza ukuzaji wa biashara hasa
ya nyama kati yake na Tanzania huku kukiwa tayari na makampuni kadhaa
ktoka Iran yanayowekeza katika eneo la Ujenzi.
Katika
ziara hiyo Mheshimiwa Makamu wa Rais pia alipata fursa ya kukutana na
Rais wa tatu wa Iran Akbar Hashem Rafsanjeni na kufanya naye mazungumzo
kuhusu mashirikiano baina ya nchi zetu mbili. Rais Rafsanjeni aliyepata
kufika Tanzania mwaka 1996 alisisitiza kuwa kuna mengi ambayo Iran
ilipanga kufanya na Tanzania mbayo yalizorota baada ya utawala wake
lakini ni imani yake kuwa yataendelea kufanyiwa kazi sasa. Baadhi ya
maeneo aliyoyajadili ni katika elimu ambapo katika kipindi chake
alianzisha kozi za Kiswahili katika vyuo vya Iran na eneo lingine likiwa
la kuwezesha upatikanaji wa viwanda vya Korosho.
Kwa
upande wa Mheshimiwa Makamu wa Rais alimueleza Rais Mstaafu Rafsanjeni
kuwa, Tanzania inatambua uhusiano wa kihistoria iliyonao na Iran na
kwamba ina nia ya dhati kuona uhusiano huo unaimarika zaidi na hasa
katika maeneo ya uwekezaji na biashara za pamoja. Rais Mstaafu
Rafsanjeni alisema kuwa Iran kwa sasa inakabiliwa na vikwazo kadhaa
ambavyo kwa namna moja ama nyingine vimekwamisha baadhi ya mambo ambayo
wao kama nchi waliyapanga kuyafanya lakini akafafanua kuwa anaona
tuendako kuna nuru hivyo mafanikio ya kutimiza makubaliano baina ya nchi
zetu yanaweza kufikiwa.
Msafara
wa Mheshimiwa Makamu wa Rais ambao pia uliambatana na Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mahadhi Maalim umeondoka leo
hapa Tehran kurejea nyumbani. “Tuna mengi ya kujifunza kutoka Iran na
uhusiano wetu wetu una kila sababu ya kudumishwa,” alimalizia Mheshimiwa
Makamu wa Rais baada ya kuagana na Rais Mstaafu Rafsanjeni na saa
chache kabla ya kurejea nyumbani.
Imetolewa na: Ofisi ya Makamu wa Rais
Tehran, Iran
Jumatatu Agosti 05, 2013
Post a Comment