Wiki kadhaa baada ya kutoroka nchini na kukimbilia
nchini Qatar kwa ajili ya kwenda kufanya majaribio ya soka la kulipwa, leo hii
kiungo wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Simba Mwinyi Kazimoto amezungumza
rasmi na mtandao huu na kutoa taarifa nzima ya kuhusu sakata lake la kutoroka.
Akizungumza
kwa njia ya simu kutoka Doha Qatar na Shaffih Dauda, Mwinyi Kazimoto kwanza
amekiri kwamba alitoroka kwenda Qatar kwa nia ya kwenda kufanya majaribio, "Safari
yangu ya kuja huku Qatar ilibidi iwe kabla hata sijacheza mechi ya marudiano na
Ivory Coast, lakini kwa sababu nilikuwa na majukumu nilivumilia nikabaki mpaka
nilipocheza mchezo wa kwanza dhidi ya Uganda, wakati tukiwa kambini kwa ajili
ya mchezo wa pili ikabidi niondoke kwa sababu siku zilikuwa zinaenda na muda
wangu wa kufanya majaribio ukawa unaisha," anazungumza Kazimoto
Alipoulizwa kama tayari ameshafuzu majaribio aliyoenda kufanya kiungo huyo wa zamani wa JKT Ruvu alisema: "Mwanzoni nilipata vilabu viwili vinavyoshiriki ligi daraja la kwanza ya huku, lakini nikachelewa majaribio na hivyo nikakosa nafasi. Baada ya hapo ndipo ikajitokeza timu ya Al-Markhiya Sports Club - inayoshiriki ligi ya daraja la pili na ikavutiwa nami na ikafanya mipango ya kunisajili."
Taarifa
nchini zimeenea kwamba klabu ya Simba imepokea kiasi cha $35,000 kwa ajili ya
kumuuza kiungo huyo, Je Kazimoto anasemaje juu ya hili? "Ni kweli
kutokana na kwamba nilikuwa na mkataba wa mwaka mmoja na Simba ilibidi nitoe
kiasi cha fedha ($40,000 na sio $35,000 kama inavyoripotiwa) kutoka kwenye ada
ya usajili wangu kuununua mkataba wangu uliobakia na Simba
"Sasa hivi nimefanikiwa tayari kupata timu hii
lakini ndoto yangu ni kujitahidi na kuweza kucheza ligi ya juu kabisa hapa.
Vilevile ningependa kuwaomba radhi watanzania wote na klabu yangu ya Simba kwa
kitendo cha kutoroka wakati nikiwa nahitajika. Nafasi ya kucheza soka la
kulipwa ilikuwa ni muhimu kwa maisha yangu na sikutaka niipoteze hivyo naomba
wanielewe na kunisamehe."
Post a Comment