Mkuu
wa Mawasiliano na Masoko wa KCB Benki Bi. Christina Manyenye (katikati)
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) pamoja na waalimu wakuu wa shule 7 za msingi jijini Dar wakati akizindua kampeni ya ‘nunua madawati 10 upate mengine 90’ kwenye makao makuu ya benki hiyo Oysterbay jijini Dar. Kulia ni Mkuu
wa Fedha ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Tanzania Bw.
Gofrey Ndalahwa na kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari
Oysterbay Mwl. Gladys Mhina.(Picha na Zainul Mzige wa Dewji Blog).
Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Sekondari Oysterbay ya jijini Dar Mwl. Gladys Mhina
akitoa shukrani kwa KCB Benki kwa kuzindua kampeni hiyo ambayo itasaidia
kuboresha mazingira mazuri ya kujisomea kwa wanafunzi nchini na pia
kuongeza ufaulu.
Sehemu ya Walimu Wakuu wa shule saba waliowakilisha shule zao kwenye hafla hiyo.
Benki ya KCB Tanzania leo imezindua rasmi kampeni ya nunua madawati 10 upate mengine 90 yaani ‘buy 10 and get 90 desks’ itakayodumu kwa muda wa mwezi mmoja na kuhusisha shule saba za serikali za Dar es Salaam.
Akizungumza
na waalimu wakuu wa shule za msingi Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa
Benki ya KCB Tanzania Christina Manyenye amezitaja shule hizo kuwa ni
Shule ya Msingi Makumbusho, Hannanasif, Sinza, Msasani B, Mbuyuni,
Mkunguni na Shule ya Sekondari ya Oysterbay.
Amesema
kampeni hii italeta ushirikiano mzuri kati ya shule hizo saba na benki
ya KCB na inazikumbusha shule hizo kwamba zinaweza kuboresha mazingira
ya elimu angalau kwa kiwango Fulani na pia inakuza umiliki wa madawati
yatakayo nunuliwa kwa ajili ya wanafunzi.
Manyenye
amesema jumla ya gharama yote ni shilingi 131,000,000/=ambapo
watakabidhi madawati 100 kwa kila shule ya msingi na madawati131 kwa
shule ya sekondari ya Oysterbay.
Aidha
amesema kusaidia jamii benki hiyo imeenda mbali zaidi, badala ya
kusaidia tu jamii kwa kutoa misaada mbalimbali pia wanayo akaunti maalum
kwa ajili ya mashirika na taasisi za kijamii yaani ‘Organizations and
Institutions with Social Impact’ inayoitwa “Community Account” ambayo
haina malipo ya mwezi ya uendeshaji (no ledger fee).
Post a Comment