KCB benki Tanzania yazindua kampeni ya ‘nunua madawati 10 upate mengine 90’ kwa shule 7 za Dar.

IMG_1629
Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa KCB Benki Bi. Christina Manyenye (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) pamoja na  waalimu wakuu wa shule  7 za msingi jijini Dar wakati akizindua kampeni ya ‘nunua madawati 10 upate mengine 90’  kwenye makao makuu ya benki hiyo Oysterbay jijini Dar. Kulia ni Mkuu wa Fedha ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Tanzania  Bw. Gofrey Ndalahwa na kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Oysterbay Mwl. Gladys Mhina.(Picha na Zainul Mzige wa Dewji Blog).
IMG_1666
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Oysterbay ya jijini Dar Mwl. Gladys Mhina akitoa shukrani kwa KCB Benki kwa kuzindua kampeni hiyo ambayo itasaidia kuboresha mazingira mazuri ya kujisomea kwa wanafunzi nchini na pia kuongeza ufaulu.
IMG_1632
Sehemu ya Walimu Wakuu wa shule saba waliowakilisha shule zao kwenye hafla hiyo.
Benki ya KCB Tanzania leo imezindua rasmi kampeni ya nunua madawati 10 upate mengine 90 yaani ‘buy 10 and get 90 desks’ itakayodumu kwa muda wa mwezi mmoja na kuhusisha shule saba za serikali za Dar es Salaam.
Akizungumza na waalimu wakuu wa shule za msingi Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya KCB Tanzania Christina Manyenye amezitaja shule hizo kuwa ni Shule ya Msingi Makumbusho, Hannanasif, Sinza, Msasani B, Mbuyuni, Mkunguni na Shule ya Sekondari ya Oysterbay.
Amesema kampeni hii italeta ushirikiano mzuri kati ya shule hizo saba na benki ya KCB na inazikumbusha shule hizo kwamba zinaweza kuboresha mazingira ya elimu angalau kwa kiwango Fulani na pia inakuza umiliki wa madawati yatakayo nunuliwa kwa ajili ya wanafunzi.
Manyenye amesema jumla ya gharama yote ni shilingi 131,000,000/=ambapo watakabidhi madawati 100 kwa kila shule ya msingi na madawati131 kwa shule ya sekondari ya Oysterbay.
Aidha amesema kusaidia jamii benki hiyo imeenda mbali zaidi, badala ya kusaidia tu jamii kwa kutoa misaada mbalimbali pia wanayo akaunti maalum kwa ajili ya mashirika na taasisi za kijamii yaani ‘Organizations and Institutions with Social Impact’ inayoitwa “Community Account” ambayo haina malipo ya mwezi ya uendeshaji (no ledger fee).

Post a Comment

أحدث أقدم