Imebainika
kuwa kifafa alichopata Chris Brown jana kilisabishwa na stress
zinazomwandama kutokana na jinsi vyombo vya habari vinavyomwandika
vibaya.
Jana TMZ waliripoti kuwa kitengo cha zima moto cha Los Angeles
kilienda kwenye studio ya kurekodia muziki baada ya mtu mmoja kupiga 911
na kudai kuwa Chris alikuwa amepatwa na kifafa. Hata hivyo Chris
aligoma kutibiwa.
Mwakilishi wa Chris anasema kifafa hicho kilisababishwa na uchovu
mkali na msongo mkubwa wa mawazo na vyote vikitokana na kesi
zinazomkabili na jinsi anavyoandikwa vibaya.
Baadaye Chris alitweet:
They won't love u until u r a memory…
— Chris Brown (@chrisbrown) August 10, 2013
‘Hawatakupenda hadi uwe kumbukumbu’

إرسال تعليق