Kufikia mwaka 2041 dini itapotea kabisa kwenye nchi zilizoendelea, asema mwanasaikolojia

black_man_praying_in_churchKwa mujibu wa mwanasaikolojia mashuhuri nchini Ireland, watu wanaoamini dini kwenye nchi nyingi zilizoendelea watakuwa wachache mno ifikapo mwaka 2041.
Utafiti kuhusu imani ya watu wanaoishi katika nchini 137 ambao umetengeneza kitabu chake kipya, umegundua kuwa upagani unazidi kuongezeka zaidi kwenye nchi zilizoendelea kutokana na utajiri.
Utafiti huo umeelezea pia imani maarufu kuwa watu wenye dini watawatawala wapagani kwakuwa wao (watu wa dini) huzaa watoto wengi.
Dr Nigel Barber amekiita kitabu chake, ‘Why atheism will replace religion,’ (Kwanini upagani utachukua nafasi ya dini).
Amesema wapagani wengi wapo kwenye nchi zilizoendelea kiuchumi na dini itapungua kwa watu kutokana na kuongezeka kwa utajiri wa mtu mmoja mmoja.
Kitabu hicho kinaandika kuwa watu hawatategemea tena nguvu za miungu kwakuwa mali walizonazo zinamaliza shida zao zote.Mwandishi huyo anadai kuwa dini inapungua si tu kwasababu watu wanakuwa matajiri bali pia ni kutokana na kuongezeka kwa ubora wa maisha, kupungua kwa magonjwa hatari, elimu nzuri na ustawi mzuri wa maisha.
Anaamini kuwa hakuna haja kubwa ya dini kwenye jamii kama za Japan na Sweden ambako watu wa kawaida tu wameridhika na watu wengi wana mali. Dr Barber amesema dini ilizalishwa na mababu zetu ambao walikumbwa na changamoto nyingi katika maisha yao.
Maelezo kwenye kitabu hicho yanasema:
‘Dini ilizaliwa kuwasaidia mababu zetu kukabiliana na woga na wasiwasi.Imani kuhusu Mungu inapungua pale ambapo watu wa kawaida wanafurahia maisha, wana usalama katika afya na mambo yao ya fedha. Hata Facebook inaiua dini sababu inatoa majibu ya woga wa dunia ambao dini haina majibu yake.’
Takwimu ya watu wasiomani uwepo wa Mungu duniani kwa mujibu wa Psychology Today
There is almost no Atheism in Sub-Saharan Africa
But there are more atheists in Europe:
64% of people are non-believers in Sweden
48% of individuals are atheist in Denmark
44% of French citizens do not subscribe to a religion
42% of Germans do not believe in a god.
By Daily Mail

Post a Comment

أحدث أقدم