
Siku chache zilizopita kulikuwa na ujumbe wa sms ukisambaa kwa njia
ya ku-forward ukisema kwamba muigazaji Zaytun Kibwana a.k.a Batuly
anaumwa sana anahitaji msaada. Kama ilivyokawaida kwa wasanii wengi kuna
utaratibu wa kusaidiana wakati matatizo kama haya. Watu wengi walijua
Batuli huyu ndiyo mwenye jina halisi la “Yobnesh Yussuph” ambaye ndiye
maarufu sana kwenye bongomovie. Kumbe kuna msanii mwingine anaitwa
Zaytun Kibwana na yeye pia anatumia a.k.a Batuly ndiyo alikuwa anaumwa.
Kutoka na sms ile watu wakaanza kupigia simu Batuli lakini majibu
waliyokutana nayo ni tofauti walivyotegemea kwasababu Batuli alikuwa
haumwi. Hiki ndicho alichosema Batuli kuhusu hii ishu, “Binti unaejiita
Zaytun Kibwana a.k.a Batuly yawezekana jina langu umelipenda sana au
umeona ndio njia ya kutokea kisanaa maana nitacomplain na kitakachofuata
utajulikana, Mimi nadhani hutafanikiwa kwa style hii uitakayo hakuna
Shortcut katika maisha. Unapotumia a.k.a yangu halafu unaoomba msaada
unategemea kupata kweli? Umetumia jina langu kila anaenitafuta namwambia
sio mimi hivyo msaada unakosa na unaonekana tapeli wakati una matatizo
unatakiwa usaidiwe, tumia akili ili upate msaada. Kutumia Nick Name yng
ni kujipotezea wakati na hutafikia malengo.”
إرسال تعليق