MGANGA WA KIENYEJI AUWAWA NA WATU WASIOJULIKANA MKOANI IRINGA.

MGANGA mmoja wa kienyeji  aliyefahamika kwa jina la George Tereva (55) amefariki dunia baada ya kupigwa risasi maeneo ya tumboni,kichwani na kwenye paji la uso kisha kukaktwa na panga kichwani na watu wawili wasiojulikana.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhani Mungi alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa moja na nusu katika kijiji cha Lungemba kata ya Lungemba wilaya ya Mufindi.

Kamanda alisema kuwa watuhumiwa wa tukio hilo wanatafutwa na jeshi la polisi na mara watakapopatikana watafikishwa kituoni uchunguzi utakapo kamilika . kamanda alibainisha kuwa chanzo cha tukio hilo hakijajulikana

Post a Comment

أحدث أقدم