Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam.
NITAMSHANGAA
Mtanzania yoyote anayeweza kufurahia nchi za Tanzania na Rwanda
kuendelea kurushiana maneno makali kuonyesha uhusiano mbaya ulioanza kwa
siku za hivi karibuni.
Tangu
Mwezi Mei mwaka huu wa 2013, baadhi ya matamko mabaya yamekuwa
yakitolewa na viongozi wa Rwanda. Wanasema mengi kuonyesha chuki zao kwa
Watanzania na rais wao kwa ujumla. Kwa
kuangalia sakata lote linaloshika kasi, ila si sababu ya Tanzania
kujibu mashambulizi dhidi ya Taifa hilo linaloongozwa na Paul Kagame,
maana ni kuzidi kukuza uhasama huo.
Ni
wazi kuwa nchi ya Rwanda inayotajwa kufadhili machafuko nchini Kongo,
hasa kwa kikundi cha M23 inaleta chokochoko kwa Tanzania, pale Rais
Kikwete, alipowataka wakae na waasi kujadili tatizo. Hali
hii inashangaza mno. Kauli ya furaha inapobadilishwa na kuwa chuki na
uhasama, tena bila sababu za msingi. Labda kuna sababu nyingine, ila si
haya yaliyozungumzwa na Kikwete.
Wakati
naangalia kwa kina mtifuano huo, kwa upande wangu nitakuwa wa mwisho
kufurahia au kuombea mabaya kwa mataifa haya mawili, yani Tanzania na
Rwanda. Tanzania
ili iweze kukua kiuchumi, inahitaji ushirikiano kutoka kwa majirani
zake. Nchi hizi zinategemeana. Rwanda wanaihitaji Tanzania na Watanzania
wanahitaji uwapo wa ndugu zao.
Sipendi
kuona uhusiano mbaya kwa nchi za Tanzania na Rwanda unakua, nikiamini
ni hatua isiyokuwa na faida zaidi ya hasara kwa mataifa haya mawili
yanayopigania kujitawala wenyewe. Katika
hotuba yake aliyoitoa mwishoni mwa mwezi uliopita, Rais Kikwete
alielezea mambo mengi dhidi ya Rwanda, akisititiza kuwa alinukuliwa
vibaya na ushauri wake kupindishwa. Rais Kikwete aliwatangazia umma kuwa hakuna sababu ya kugombana na Rwanda, japo alikiri kutukanwa na majirani zetu hao.
Haya
ni matatizo makubwa kwa viongozi wa Afrika. Kagame, akiwa kama rais wa
Rwanda, ni vyema akazingatia nidhamu katika utawala wake. Kagame
anapaswa kujua faida ya amani inavyoweza kuwafanya wananchi wake waishi
vizuri. Wananchi wa Rwanda wasingependa kuona wapo viongozi wanaotamani
kulifanya Taifa hilo liingie kwenye hatari.
Kadhia
waliyoipata mwaka 1994 inatosha. Roho za Rwanda ziliangamia bila
sababu. Kama hivyo ndivyo, nani anaweza kusimama hadharani akachochea
vita, huku akijua kuwa hana faida navyo? Nani
anayeweza kuelezea faida ya vita, hasa kwa Tanzania na Rwanda, ambazo
zenyewe zinahitaji kuishi kwa kutegemea wahisani, Mataifa makubwa? Huu
si wakati wa kujenga uhasama. Huu ni wakati wa viongozi wa nchi za
Afrika kukaa pamoja na kusema kwa kauli moja namna ya kuyasaidia mataifa
yao.
Mrwanda apinge kwa nguvu zote kama kuna chokochoko zinazofanywa, zinazotakiwa kufanywa na viongozi wao leo au kesho. Mtanzania,
Mkenya, Mburundi, Mkongo na wengine wote wapinge kama kuna anayetaka
kumsumbua mwenzake kwa namna moja ama nyingine. Inawezekana
wakati mwingine kunatokea migongano ya kimaslahi, ila hakuna ugomvi
usiokuwa na njia ya kusuluhishwa. Mazungumzo mara kadhaa huleta tija na
kudumisha jamii bora.
Hakuna
nchi iliyoendelea kwa kupenda vita, hasa hizi zinazoishi kwa misaada
kutoka nchi za watu. Ukiacha roho za watu zinavyoangamia katika
machafuko, pia nchi zinatumia gharama kubwa kujilinda au kujibu
mashambulizi au kununua silaha kwa fedha za kujenga shule, vituo vya
afya na huduma nyingine muhimu kwa wananchi wao.
Rais
Kikwete ameyaona haya. Na kutokana na ustahimilivu wake, akabaini kuwa
hakuna sababu ya maana ya kulumbana na Rwanda, sababu ikiwa kuwashauri
kumaliza tofauti zao na waasi. Kauli
hii haikuungwa mkono na Kagame. Maneno ya kejeli yakaanza kushika kasi,
sambamba na vijana wao, ikiwa ni njia ya kufikisha matusi kwa
Watanzania kwa njia mbalimbali, ikiwamo mitandao ya kijamii.
Ukiingia
katika mitandao mbalimbali na kufuatilia uhasama huu, utagundua kuwa
umefikia wakati mbaya mno. Inahitaji moyo mno kujitangaza kuwa wewe ni
Mtanzania mbele ya Mrwanda. Hii
si njia nzuri kwa mataifa haya. Nchi ya Tanzania amani ni jambo la
lazima kwa wananchi wake. Ingawa ina makabila zaidi ya 120, ila yameishi
kwa upendo wa hali ya juu.
Wanapokutana
Wazigua na Wasukuma, huwezi ona tofauti yao. Wanaishi kama ndugu.
Huwezi kuona malumbano kati ya Wangoni na Wachaga. Haya ni mambo ya
kupongezwa na Watanzania wote. Amani
hii ni tunu kutoka kwa Mungu. Ingawa hatuna utajiri wa kupindukia, ila
maisha yetu yamekuwa na furaha tele, jambo linalotangaza sisi ni nani.
Kwasababu
hiyo, yoyote anayeona ana hamu ya kulichanganya Taifa hili, basi
aangalie mara mbili. Japo uwezo wa kufanya lolote upo, lakini nini
chanzo? Chanzo
kiwe hiki cha viongozi kushauriana? Kwani kuna ulazima kufuata ushauri
ambao huutaki? Kwanini sasa ubabaike kwa kushauriwa?
Alipokuwa
Tanzania katika ziara yake, Rais wa Marekani, Barrack Hussein Obama,
aliulizwa juu ya machafuko yanayoendelea nchini Kongo. Obama alijibu huku akionyesha kuwa rais wa Tanzania, Kikwete, ana uwezo wa kuyafanyia kazi hayo, maana yapo ndani ya uwezo wake.
Kauli
hii sio tu imemjenga Kikwete nje ya mipaka yake, pia imeonyesha namna
gani Watanzania wanaongozwa na rais mwenye mtazamo wa kina. Haya
yanapotokea, kwa rais asiyejitambua, rais mwenye ubinafsi na ubabe
usiokuwa na tija, ana uwezo wa kuchukia kama inavyoonekana sasa.
Anawaza
kwanini asiwe yeye? Na inapotokea mmoja wapo, ikiwamo Rwanda inaanzisha
chokochoko, kama mmoja wao anakuwa hajitambui, uhasama huo
utaongezeka. Ni
vyema wananchi wakapinga kwa nguvu zote kama viongozi wao wanataka
kuwaingiza kwenye uhasama. Watu zaidi 500,000 waliripotiwa kupoteza
maisha katika mauaji ya kimbari mwaka 1994.
Ni
idadi kubwa mno. Sitarajii kuona vifo hivyo vimesahauliwa na wananchi
sambamba na viongozi wao. Ndio maana nasema, suala la machafuko si la
kuchekea. Linazalisha
vizazi tegemezi. Linazalilisha watu kwa kiasi kikubwa mno, hivyo
halistahili kuchekewa. Watu wanazikimbia nchi zao bado wanazipenda.
Akina
mama wajawazito na watoto ndio wanakuwa wahanga wakubwa katika hilo.
Wengine wanapoteza maisha kutokana na njaa, shida ya maji na mengineyo. Wengine
wanaingiliwa kimwili bila lidhaa yao. Kama haya yanatokea, nani
anaumia? Ni wakati sasa wa viongozi wa Afrika kudumisha umoja na
mshikamano.
Hakuna
Tanzania, Rwanda, Kongo, Burundi, Kenya, Msumbiji ama Uganda. Hizi nchi
zote zinapaswa kuishi kwa upendo na kushirikiana kibiashara. Hatuhitaji
uhasama wa aina yoyote kutoka Rwanda, kama njia ya kukuza uchumi wa
nchi hizi mbili. Wapo baadhi yao wanaochekea machafuko.
Hawa
wameshindwa kung’amua machungu wanayokutana nayo wana jamii wengine
kutokana na matokeo hayo. Mwisho kabisa, napongeza kwa nguvu zote kauli
ya Rais Kikwete, nikiamini kuwa ni mwenye busara. Pamoja
na matusi yote anayotukanwa, akidhalilishwa, ila yeye anaona hakuna
sababu ya kujibizana vibaya na majirani zao hao, japo uwezo huo upo.
Rwanda
ni Taifa dogo mno. Kinguvu halina ubavu hata robo ya kupambana na ubavu
wa Tanzania. Na wenyewe wanajua hilo. Hata hivyo hakuna sababu kubwa
juu ya suala hilo. Muhimu
ni viongozi wa nchi zote za Afrika kupendana, kuhubiri amani katika
vikao vyao, maana ndivyo vinavyoweza kuleta maendeleo kwa nchi zao.
Watanzania
tunawapenda na kuwaheshimu majirani zetu, japo sio sababu ya kuonekana
si lolote, maana tunajua uwezo tunao, tena mkubwa mno.
+255 712053949
إرسال تعليق