"MIILI ya askari wawili wa Kituo cha Polisi cha mjini Namanyere wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Konstebo John Mkoma (26) mwenye nambari H1 na Benjamin Justine (27) mwenye nambari G 9696 imesafirishwa kwenda makwao kwa maziko.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob
Mwaruanda alithibitisha leo kuwa, tayari miili hiyo ya askari hao vijana
imesafirishwa jana jioni kwenda vijijini kwako kwa mazikom .
Aliongeza kuwa mwili wa Kontebo Mkoma
umesafirishwa kwenda kijijini Msangano wilaya mpya ya Momba mkoani Mbeya
ambapo mwili wa Konstebo Benjamin umesafirishwa kwenda kijijini Hedaru
mkoani Kilimanjaro kwa maziko .
Kwa mujibu wa Mwaruanda askari hao
walikufa baada ya kugongwa na gari linalodaiwa kuwa katika mwendo kasi
Alhamisi wiki hii saa mbili za usiku usiku mjini Namanyere katika
barabara ya kutokea Soko Kuu kwenda katika Kituo hicho cha Polisi kikazi
.
Alibainisha kuwa ajali hiyo ya barabara
ilihusisha pikipiki yenye namba za usajili T 903 DUP mali ya Mkoma
aliyekuwa amempakia mwenzake, na gari aina ya Toyota Hiace lenye namba
za usajili T 875 CJC, mali ya Kaimu Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Nkasi,
Simon Salala (31) ambaye ndiye aliyekuwa akiendesha gari hilo.
Akielezea tuko hilo, Mwaruanda alisema
usiku huo polisi walikuwa wakielekea kazini, lakini ghafla waligongwa na
Salala aliyekimbia na gari hadi nyumbani kwake na yeye mwenyewe kwenda
kujificha,lakini baada ya msako alikamatwa na sasa na sasa anashikiliwa
na jeshi polisi.
إرسال تعليق