Msanii
wa vichekesho Mkono wa Mkonole anatarajia kuachia wimbo wa gospel
comedy uitwao ‘Nimepona’ alioimba na wachekeshaji wenzie, Kiwewe na
Matumaini ili kutoa burudani ya uchekeshaji sambamba na kumuabudu Mungu.
Ujio wa wasanii hao na wimbo wa ‘Nimepona’ umekuja baada ya wasanii
hao kujadiliana na kugundua pia kupitia uchekeshaji wanaweza kumshukuru
Mungu kwa kupitia kipaji cha uchekeshaji ambacho wamepewa na Mungu na
pia kuonyesha ni jinsi gani wanaweza kuitumia sanaa yao kufikisha ujumbe
kwa jamii.
“Sisi ni wasanii na ni kioo cha jamii kwahiyo tunapenda kuwajulisha
ndugu watanzania, wapenzi wa burudani pamoja na wadau wote wa muziki wa
injili kuwa mkae tayari kwa kupokea nyimbo mpya inayoitwa Nimepona
ambayo imeandaliwa kutoka katika kundi la ‘Comedian Gospel’ linaloundwa
na Mkono wa Mkonole, Kiwewe na Matumaini, Mkono wa Mkonole aliambia
Bongo5.
إرسال تعليق