Mpya Kutoka Kwa Izzo Buzness 'Love Me Dance' Inakuhusu Shabiki Wa Kweli

Msanii wa muziki wa kizazi kipya hapa Bongo, Izzo Business ambaye kwa sasa kazi yake inayokwenda kwa jina Love Me inafanya vizuri kwenye chati mbalimbali, katika hatua ya kujisogeza karibu na mashabiki wake na pia kuitangaza kazi hii zaidi, ameamua kuanzisha mpango unaokwenda kwa jina Love Me Dance.
Mpango huu ni kwaajili ya mashabiki wa msanii huyu wa jinsia zote ambao wataweza kushiriki kwa kumtumia picha wakiwa katika pozi la 'love me dance' ambalo mfano wake ni kama inavyoonekana katika picha inayofuata hapa chini, na hizi zitatumwa katika anuani ya msanii huyu ambayo ni lovemedanceizzo@gmail.com.

Picha hizi Izzo atazipatia shavu la kuzi-post katika page yake na kuziwezesha kuonekana na watu wengi zaidi. 

Post a Comment

Previous Post Next Post