Mkurugenzi
Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Usu Mallya (wa
kwanza kushoto) akizungumza na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya
habari katika mkutano na wahabari hao leo kwenye ofisi za mtandao huo
Mabibo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi
Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bi. Usu Mallya (wa pili
kulia) akizungumza na wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari.
Alioambatana nao ni viongozi anuai, watendaji na baadhi ya wanachama wa
TGNP. katika mkutano na wahabari.

Sehemu
ya jopo la viongozi na wanachama wa TGNP wakiorodhesha maswali ya
wahariri (habapo pichani) kabla ya kuanza kuyatolea majibu kwenye
mkutano huo leo.


Meneja wa Idara ya Habari na Mawasilino TGNP, Lilian Liundi (wa pili kushoto) akifafanua jambo katika mkutano na wahariri



Baadhi ya wahariri kutoka vyombo anuai vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa katika mkutano na TGNP

Baadhi ya wahariri kutoka vyombo anuai vya habari jijini Dar es Salaam wakiwa katika mkutano na TGNP

Baadhi ya wahariri wakifuatilia mkutano huo na viongozi, watendaji na wanachama wa TGNP.
Katika
mkutano huo na wahariri TGNP imeainisha baadhi ya mafanikio na
changamoto ambazo mtandao huo umezipata, ikiwa mbioni kufanya tamasha la
mwaka huu ambalo litafanyika Septemba 3 hadi 6 2013, Katika viwanja vya
TGNP Mabibo.
TGNP
inatarajia kutumia Tamasha la Jinsia kuwapa wanawake fursa ya kushiriki
mijadala ya wazi na kupaaza sauti zao, tamasha hili litashirikisha
wanawake, wanaume, Vijana na watoto zaidi ya 5000 kutoka mikoa yote ya
Tanzania na nchi mbalimbali za Afrika, Ulaya na Amerika.
TGNP
imebainisha kuwa kupitia Tamasha hilo, wanawake na wanaume wanaoshiriki
wanapata fursa ya kujijengea uwezo wa kutumia mbinu za kiraghibishi
katika, uchambuzi wa sera , bajeti ya kijinsia, kujadili kwa pamoja na
watendaji wa serikali kuu na za mitaa walioalikwa namna bora ya utoaji
huduma ambazo zitamfikia kila mwananchi.
Pamoja
na mijadala hiyo ya wazi, kutakuwa na mahakama ya wananchi (Popular
tribunal) itakayoendeshwa na Chama cha Majaji Wanawake (TAWJA), watunga
sera, wanasheria, wanaharakati waliobobea kwenye masuala ya Kisheria na
wananchi walioathiriwa na mfumo kandamizi na kukosa msaada wa kisheria
au kuathika na hukumu zilizotolewa. Aidha siku inayofuata kutakuwepo na
Bunge la wananchi ambalo litaongozwa na wanazuoni na wataalamu wa sheria
na wananchi wote watapata fursa ya kushiriki kikamilifu.
Mijadala
mingine italenga katika masual ya haki ya uchumi kwenye upatikanaji wa
huduma za msingi za jamii kama maji, afya, elimu, miundombinu na haki ya
jamii katika umiliki wa rasilimali ardhi. Aidha suala la Katiba mpya
litapewa kipaumbele katyika mijadala itakayopfanyika ikiwepo kuendelea
kudai ushiriki ulio sawia katika fursa na michakato iliyosalia kufikia
kupata katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Post a Comment