MTOTO mchanga wa kike wa eneo la Sabasaba wilayani Tarime Mkoa wa Mara, Maria Samwel anatakiwa kuhamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando ya jijini Mwanza kwa ajili kuondolewa uvimbe wa ajabu uliopo kisogoni.
Mganga Mfawidhi wa Wilaya, Dk. Marco Nega alimwambia mwandishi wetu kuwa walifikia uamuzi wa kumhamishia mtoto huyo Hospitali ya Rufaa ya Bugando baada ya kubainika kuwa tatizo lake hilo ni kubwa.
“Mtoto huyu alizaliwa na tatizo hilo Julai 14, mwaka huu na atakwenda kutibiwa bure Bugando ili kuokoa uhai wake,” alisema Dk. Nega.
Mwandishi wetu alizungumza na baba mzazi wa mtoto huyo, Samwel Ryoba, mkazi wa Sabasaba mjini hapa akasema mwanaye anahitajika kufanyiwa upasuaji lakini walichelewa kumpeleka Bugando kutokana na ukata.
‘’Tumechelewa kumpeleka mtoto wetu Bugando ili akaondolewe tatizo hilo kwa kupasuliwa kutokana na kukosa fedha za matumizi wakati tukiwa Mwanza licha ya kuambiwa kuwa mtoto atatibiwa bure.
Mama mzazi wa mtoto huo, Kegocha Samwel Ryoba alisema kuwa muda wote wakati wa ujauzito wake alikuwa akihudhuria kliniki hadi hatua ya mwisho ya kujifungua, akashangaa kuona mwanaye ana tatizo hilo na ameomba kusaidiwa.
Wanaoguswa na habari hii wanaweza kutuma fedha kwa namba 0788-218682.
-Risasi, via GPL
Post a Comment