Mtoto
wa kiume wa Usher, Usher Raymond V mwenye umri wa miaka mitano
amelazwa hospitali baada ya kupata ajali kwenye bwawa la kuongea jana.
Vyanzo vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa ajali hiyo ilitokea mida ya saa
12 jioni. Mtoto huyo alipelekwa moja kwa moja ICU kwenye hospitali ya
jijini Atlanta. Usher hakuwepo nyumbani wakati wa tukio hilo.

Kutokana na ajali hiyo imedaiwa kuwa mapafu yake yalijaa maji. Usher
Raymond V, ambaye Usher humwita Cinco, ni mtoto wa kwanza aliyezaa na
mke wa zamani Tameka Raymond. Wazazi hao wote wapo hospitali kufuatilia
afya ya mtoto wao.
Mwaka jana mtoto wa mke wake huyo wa zamani, Kile alifariki kutokana na kugongwa na boti.
إرسال تعليق