Siku
kama ya leo miaka 27 iliyopita, Miss Tanzania 2005 na Miss World
Africa, Nancy Sumari alizaliwa. Nancy ambaye ni mama wa mtoto mmoja wa
kike, Zuri amefanya interview exclusive na Bongo5 kuhusu birthday yake.
Kuhusu kitu kikubwa anachoshukuru kwa mwaka aliopita
Ni mafanikio makubwa na blessings nyingi ambazo nimezipata. Kuwa na
uwezo tu wa kuja kazini kila siku, kufanya kazi na timu ambayo imesimama
kufanya kazi na wadau, sponsors, kuweza kuandika kitabu na kukipublish
na kukisubmit wizarani, blessings ni nyingi sana. Ninapata support kubwa
sana kutoka kwa familia yangu, rafiki zangu, yaani ni mtu ambaye nina
mengi ya kumshukuru Mungu kwakweli.
Kuhusu kitu kikubwa anachokiona katika umri alionao sasa
Ni mabadiliko tu ya muonekano wa maisha. I think unavyoendelea kuwa
mtu mzima vitu vinabadilika. Kwangu nyumbani ni muhimu zaidi kuliko
sehemu yoyote nyingine. Siku za nyuma yaani kwenye ujana ikifika Ijumaa
ni kitu cha kitaa. So sasa hivi vitu ambavyo naviona ni muhimu
vimebadilika sana, I think ndio utu uzima huo, utu uzima dawa.
Kuhusu anachotazamia kufanya mwaka huu, kama mama, mwanafunzi na kama Mkurugenzi Mtendaji wa Bongo5
Katika kila Nyanja natarajia kufanya mabadiliko chanya kwenye jamii.
Kama mama ningependa kumlea mtoto wangu kwenye maadili ambayo mimi naona
yapo sahihi na pia kusukuma hiyo meseji kwa wazazi walio wengi zaidi,
maybe kupitia blog yaani kushare experience zaidi na kujifunza pia kwa
wazazi wenzangu ili kuiendeza jamii yetu ikue kwa maadili yaliyo joint,
yanayoweza kuwaendeleza watoto wetu ili tuwaone wao in the future
wanakuaje kutokana na malezi yetu sisi. Kama mwanafunzi, ofcourse ndio
namalizia chuo kwahiyo niko very excited, Mungu amenisaidia naendelea
kufanya vizuri.
Kama MD, kama ilivyo jadi yetu ni kuendelea kwenda mbele zaidi,
kusukuma mipaka kwenye burudani, kwenye social entrepreneurship, kwenye
entertainment, yaani kila nyanja ambayo tunaiguza. Tunataka tuwe mbele
zaidi na tunataka tufike miaka 10 kabla ya wenzetu.
Kuhusu kumbukumbu nzuri zaidi ya birthday aliyonayo
Nadhani ilikuwa mwaka juzi ambapo ndio birthday yangu ya kwanza
nilikuwa na mtoto wangu, nikawa na mwenzangu. Tulisherehekea kwa pamoja
kama familia. That was the first birthday ambayo nilihisi my life is
complete.
Kuhusu kama anategemea kufanya kitu kikubwa kwenye birthday yake leo
Kuhusu kama anategemea kufanya kitu kikubwa kwenye birthday yake leo
Sitegemei kufanya kitu kikubwa sana. Ni kutoa tu shukrani kwa friends, kusherehekea na family kidogo.
Kama amewahi kuchukia baada ya mtu wake wa muhimu kusahau birthday yake
Huwa hawasahau kwasababu ni wajanja kwa mfano leo nilitegemea wazazi wangu wangesahau, kaamka asubuhi mdogo wangu kawapigia simu, yaani kukumbushana so hawajawahi kuharibu na nawashukuru kwa hilo.
Huwa hawasahau kwasababu ni wajanja kwa mfano leo nilitegemea wazazi wangu wangesahau, kaamka asubuhi mdogo wangu kawapigia simu, yaani kukumbushana so hawajawahi kuharibu na nawashukuru kwa hilo.
Kuhusu kama amewahi kuamka asubuhi na akasahau birthday yake hadi alipokumbushwa
I think wakati ule nipo boarding shule manaake kila siku zinafanana.
So hiyo siku nimeamka nikawa nimesahau kabisa. Mawazo yote yapo kwenye
issue nyingine tofauti sio birthday lakini after that haijawahi kutokea
kwakweli kwasababu ni siku muhimu kwangu.
Kuhusu nani amekuwa mtu wa kwanza kumtakia birthday njema
Zuri na baba yake wamekuwa wa kwanza yaani tangu wiki iliyopita
wameanza kuniwish happy birthday. Kwasababu alikuwa anajibu kumfundisha
yaani Zuri aanze kuimba happy birthday so wao ndio walikuwa wa kwanza
then friends ndio wakafuatia yaani watu wote ambao wananijali na mimi
nawajali nadhani leo wamefikisha ujumbe so it’s very special.

Nancy na Zuri kwenye kava la jarida la Bang
Kuhusu kama ameweza kujibu wishes zote anazopata kwenye Twitter
Najitahidi nizijibu zote kwasababu nahisi mtu akiwa amechukua effort
yake kukukumbuka akakuwish yaani ni furaha tu so najitahidi najibu zote.
Kuhusu anachotarajia kupata kwa dinner leo?
I think itakuwa something simple, something small. Mimi kawaida
napenda vitu ambavyo viko small, simple yaani mnasherehekea lakini at
the same time mnakuwa thankful.
Nyimbo tatu anazopenda kusikiliza leo
Naomba unichagulie Top 3 ya Marimba Music Chars ya wiki iliyopita.

إرسال تعليق