Hatujathibitisha
bado lakini tunahisi kuna ‘trouble in Paradise’. Leo Nay wa Mitego
amekuwa akiandika ujumbe wenye mafumbo kwenye Instagram na baada ya
kuusoma ndani ya mistari (read between the line) tumegundua huenda mambo
si mazuri kati yake na mpenzi wake ambaye hivi karibuni alikuwa
akitarajia kumzalia mtoto lakini mimba ikaharibika.
Nay ambaye jina lake halisi ni Emmanuel Munisi, ameanza kwa kuandika
ujumbe huu: Sasa mapenzi basi# by diamond Platnumz..!! Single boy# Ally
Kiba#966’

Baada ya muda kidogo ameandika tena:
Niko ivi,,, nikikupenda nakupenda kwa asilimia 100# na kila m2 atajua
juu ya upendo wangu kwako..!! Bt ukizingua nakuacha na ninakusahau kwa
asilimia 200# na kwa muda mchache 2. Nikiamua huwa sirudi nyuma..!!#
Mwanamke mjinga ataivunja ndoa yake kwa mikono yake ye mwenyewe# by
Linex.#966’
Tunahisi mambo si mazuri kwenye ulimwengu wa mapenzi wa Nay, Itafahamika.
إرسال تعليق