Ndege ya kijeshi imelipuka na
kuteketea nchini Somalia baada ya kutua kwa dharura katika uwanja wa
kimataifa wa ndege mjini Mogadishu.
Kikosi cha muungano wa Afrika nchini Somalia
ambacho kina kambi yake katika uwanja huo wa ndege kimesema kuwa
wanajeshi wake kadhaa wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa.Kuna ripoti kuwa ndege ilikuwa imebeba zana za kivita.
Wafanyakazi katika uwanja huo wa ndege walielezea kusikia milipuko kadhaa huku moto ukienea kwa ndege hiyo.
Ndege za kijeshi hutua katika uwanja huo wa ndege unaotumiwa na wanajeshi wa muungano wa Afrika wanaopambana dhidi ya wapiganaji wa Al shabaab wanaosemekana kuwa na uhusiano na al Qaeda.
Wakati huohuo, kwenye mtandao wao wa Twitter kundi la Al Shabaab limeeleza kufurahia kwa kulipuka kwa ndege hiyo hasa kwa kuwa ililipuka yenyewe.
Kwenye ujumbe mwingine , kundi hilo lilisema kuwa ndege hiyo iliyokuwa imebeba silaha iliteketea katika uwanja wa Mogadishu na kuharibu kila kilichokuwa kwenye ndege yenyewe.
Kundi hilo lililaumu ilichokiita watu waliolaaniwa kwa kupanga mauaji ya waumini na kufanya uharibifu lakini kila wanachokifanya, juhudi zao zinagonga mwamba.
إرسال تعليق