Msanii wa Hip Hop Bongo,Elibarik
Emaniel‘Nay wa Mitego amefunguka kuwa kama akifariki dunia hataki
aundiwe kamati za ajabu ajabu za wasanii wenzake wa muziki huo kwani
wengi wao hutumia kamati hizo kama mitaji kwa kutafuna pesa za
rambirambi.
Akifunguka
kupitia account zake za facebook na instragram alisema kuwa kuna baadhi
ya wasanii wanasubiri wenzao wafe ili waunde kamati ili waweze
kuzitafuna pesa kama ilivyokuwa kwenye msiba wa marehemu Albert
Mangwea‘Ngwea’.
Aidha amefunguka kuwa ameamua
kuzungumza hivyo baada ya kupokea vitisho kutoka kwa baadhi ya
wasanii,baada ya kuwadis kupitia ngoma yake aliyoiachia ya Salaam Zao
kuwa waliochukua pesa za rambirambi za Ngwea warudishe hata kimya kimya
kwani muda wanao.
‘Zipo nyingi zingine za
vitisho,nitazipost zote watu wangu mujue leo nimeanza na hiyo…! Ukweli
unauma sana siogopi vitisho vyenu…pelekeni hela za marehemu hata
kimyakimya bado nafasi mnayo,,,mi nikifa sitaki kamati za kwenye msiba
wangu maana watu wanafanya misiba yetu mitaji yao’alisema Nay.
-
إرسال تعليق