Benki
ya NMB, wiki iliyopita ilizindua taasisi ya maendeleo ya Kilimo nchini
Tanzania.Taasisi ambayo inakusudi la kuinua sekta ya kilimo kwa kuanzia
ngazi ndogo kabisa inayomgusa mkulima mdogo hadi ngazi ya wakulima
wakubwa na kilimo cha biashara.
Wakulima wadogo wadogo wamekua hawatambuliki kutokana na kutokua na
mtaji wa kutosha na uwezeshwaji kutokuwepo.Hivyo Benki ya NMB kwa
kupitia taasisi hii itawasaidia wakulima kwa kupitia vyama au vikundi
ili kuwezeshwa katika uzalishaji na kuinua sekta nzima ya kilimo.
Mkuu wa Shughuli za Kilimo wa Benki ya NMB, Robert Pascal akitoa maelezo juu ya Taasisi hiyo namna itakavyofanya kazi na kua msaada mkubwa kwa wakulima kabla ya uzinduzi uliohudhuriwa na baadhi ya wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya,Wakulima na wadau wa kilimo
Baadhi ya wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya mbalimbali mbali nchini na wadau wa Kilimo wakifuatilia Hotuba ya Afisa Mtedaji Mkuu wa Benki ya NMB, Mark Wiessing (kulia)
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB, Prof. Joseph Semboja akitoa neno la shukrani kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji Dk. Mary Nagu (katikati) baada ya kuzindua taasisi ya Maendeleo ya Kilimo ya Benki ya NMB mjini Dodoma . Wengine kutoka kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Rehema Nchimbi,C.E.O wa NMB, Mark Wiessing na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Maendeleo ya Kilimo ya Benki ya NMB, Vallerian Fernandos
Meneja Mawasiliano wa Benki ya NMB,Josephine Kulwa akimsikiliza kwa makini Mhe. Dk. Mary Nagu kabla ya hafla ya uzinduzi kuanza kati kati ni Meneja wa NMB kanda ya Kati Ole Loibanguti
إرسال تعليق