Mkurugenzi
wa Kampuni ya kizalendo ya Kotes (T) Ltd, Max Komba (wapili
kulia-waliosimama), akikagua uchimbaji mtaro kwa ajili ya kutandika
nyanya za mfumo wa mawasiliano kwenye kituo cha Polisi Oysterbay, Dar es
Salaam, jana, kuunganisha kwenye mkongo wa mawasiliano wa taifa. Kulia
ni Mhandisi wa masuala ya ICT, Makao Makuu ya Polisi, Mosses Maganza na
watatu ni mhandisi wa Kotes (T) Ltd, Mohamed Sibuga.
HABARI KAMILI
DAR ES SALAAM, Tanzania
JESHI
la Polisi nchini limechukua hatua za kujiimarisha zaidi katika
kuukabili uhalifu kisasa zaidi kwa kuamua kuviunganisha vituo vyake
vikubwa kwenye mtandao wa mawasiliano katika mkongo wa taifa.
Kufuatia
hatua hiyo, ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano hayo ya kuunganishwa
kwenye mkongo wa taifa wa mawasiliano, umeshaanza kwenye vituo vikubwa
vya polisi katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Kilimanjaro, Zanzibara na
jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari, jana, Mkurugenzi wa Kampuni ya Kotes (T)
Limited iliyopewa na jeshi la polisi kutengeneza mindombinu hiyo, Max
Komba, alisema, ujenzi huo ulianza kwenye Kituo cha Polisi Kurasini,
Chuo Cha Polisi Chang’ombe na Oysterbay ambako ujenzi wake ulitarajiwa
kukamilika jana.
Komba
alisema, kampuni yake imepewa kufanya kazi katika mikoa hiyo kwa wiki
tatu, tangu ilipoanza Julai 27 mwaka huu kwa mujibu wa mkataba, na
ujenzi unatakiwa ume imekamilika ifikapo Agosti 20 mwaka huu.
Likizungumzia
mradi huo, Jeshi la Polisi kupitia msemaji wake, lilisema, mradi huo
ukikamilika utasaidia jeshi hilo kupunguza gharama na muda mwingi ambao
limekuwa likilazimika kutumia katika kufuatilia kumbukumbu katika
kuwatambua wahalifu.
Msemaji
wa Jeshi hilo, Advera Senso, alisema, kupitia mtandao huo, vituo
vilivyounganishwa vinaweza kupata taarifa na kuziona kwa wakati mmoja na
kwa haraka zaidi, jambo ambalo litawezesha kumbaini mhalifu haraka
zaidi na kuwa na ushahidi wa kutosha baada ya kumnasa.
“Mradi
huu ni miongoni mwa maboresho mengi tunayofanya katika jeshi la polisi
ili kwenda na wakati. Hivyo baada ya kukamilisha kwenye vituo vyenye
hadhi ya mikoa kipolisi, tunatarajia pia kushuka hadi ngazi za wilaya
kulingana na mahitaji”, alisema.
Post a Comment