Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
akihutubia Wananchi katika Baraza la Idd lililofanyika Ukumbi wa Salama
Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.
Mufti
wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaab akiomba dua baada ya kumaliza hutba
ya Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein aliyoitoa katika Baraza la
Idd Bwawani mjini Zanzibar,kulia ni Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif
Ali Idd.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
akitoa Mkono wa Idd kwa Watoto na Watu wasiojiweza katika hafla
iliyofanyika Ofisi kwake Ikulu mjini Zanzibar.
Katibu
Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Zanzibar Dkt. Abdulhamid Mzee kushoto na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud pamoja na
Viongozi wengine wakipata Dhifa iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar Dkt.
Ali Mohamed Shein baada ya Baraza la Idd Bwawani mjini Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
kulia akipata Dhifa aliyoindaa baada ya Baraza la Idd huko
Bwawani,katikat ni Makamu wa Kwanza wa Ris Maalim Seif Sherif Hamad na
kushoto ni Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Aman Abeid Karume.
Baadhi
ya Viongozi na Wananchi waliohudhuria Baraza la Idd wakimsikiliza Rais
wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein aliyoitoa leo huko Hoteli ya Bwawani
mjini Zanzibar. Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
======== ========= =============
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
amesisitiza kuwa Serikali itafanya kila iwezalo kuwakamata na kuwapeleka
katika Vyombo vya sheria Watu waliohusika kuwamwagia Tindikali Raia
wawili wa Uingereza hivi karibuni.
Amesema
Vyombo vya Ulinzi na Usalama viko Imara na kwamba vitaendelea kulinda
amani ya Nchi ikiwemo kuwabaini Wahalifu wote na kuwapeleka katika
Vyombo husika. Dkt Shein ameyasema hayo leo alipokuwa akiwahutubia
Wananchi kupitia Baraza la Idd lililofanyika Ukumbi wa Salama Hoteli ya
Bwawani mjini Zanzibar.
Amesema
kwa mara ya pili kila inapokaribia Sherehe za Sikukuu kumekuwa na
mfululizo wa Matukio ya kihalifu na kuongeza kuwa kila aliyehusika hatua
za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. “Vitendo hivi si uungwa ni
Ukatili, hatutawatia hatiani Wasiohusika lakini kila aliyehusika
hatutamsamehe” Alionya Dkt Shein.
Aidha
Dkt. Shein amelaani kushamiri kwa Vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia
ikiwemo ubakaji hasa kwa Watoto ambapo jumla ya Watoto wakike 480
Zanzibar wamebakwa katika kipindi cha mwezi Julai 2012 hadi Aprili mwaka
huu.
Amesema
hilo ni jambo la kushtua sana na kwamba wakati umefika kila mmoja
kuchukua hatua zinazofaa kudhibiti hali hiyo. Dkt Shein ametoa wito kwa
Wananchi na Viongozi wote kuendelea kupendana bila kuchukiana na kulinda
Amani, Umoja na Kuvumiliana kwa manufaa ya Zanzibar.
Amesema
panapotokea tofauti za hoja kuhusu suala la Maendeleo ya Nchi jambo la
busara ni kuzungumza na kujadili kwa kuzingatia sheria zilizopo kwa
manufaa ya Zanzibar. Dkt Shein ametoa Shukrani kwa Jeshi la Polisi kwa
kudumisha hali ya amani katika kipindi chote cha Mwezi wa Ramadhani na
kulitaka Jeshi hilo lizidishe juhudi zake kipindi cha Sherehe za Idd na
siku za usoni.
Kabla
ya Baraza la Idd Dkt Shein alitoa Mkono wa Idd kwa Wazee na Watu
wasiojiweza katika hafla iliyofanyika Ikulu mjini Zanzibar.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
Post a Comment