RAIS dkt SHEIN AHUTUBIA BARAZA LA IDD LEO.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akihutubia Wananchi katika Baraza la Idd lililofanyika Ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar. 
 Mufti wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kaab akiomba dua baada ya kumaliza hutba ya Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein aliyoitoa katika Baraza la Idd Bwawani mjini Zanzibar,kulia ni Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd. 
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akitoa Mkono wa Idd kwa Watoto na Watu wasiojiweza katika hafla iliyofanyika Ofisi kwake Ikulu mjini Zanzibar.
 Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Zanzibar Dkt. Abdulhamid Mzee kushoto na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud pamoja na Viongozi wengine wakipata Dhifa iliyoandaliwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein baada ya Baraza la Idd Bwawani mjini Zanzibar. 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kulia akipata Dhifa aliyoindaa baada ya Baraza la Idd huko Bwawani,katikat ni Makamu wa Kwanza wa Ris Maalim Seif Sherif Hamad na kushoto ni Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Aman Abeid Karume.


Baadhi ya Viongozi na Wananchi waliohudhuria Baraza la Idd wakimsikiliza Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein aliyoitoa leo huko Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar. Picha zote na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
========    =========  =============
Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar  

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein amesisitiza kuwa Serikali itafanya kila iwezalo kuwakamata na kuwapeleka katika Vyombo vya sheria Watu waliohusika kuwamwagia Tindikali Raia wawili wa Uingereza hivi karibuni.

Amesema Vyombo vya Ulinzi na Usalama viko Imara na kwamba vitaendelea kulinda amani ya Nchi ikiwemo kuwabaini Wahalifu wote na kuwapeleka katika Vyombo husika.  Dkt Shein ameyasema hayo leo alipokuwa akiwahutubia Wananchi kupitia Baraza la Idd lililofanyika Ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar.

Amesema kwa mara ya pili kila inapokaribia Sherehe za Sikukuu kumekuwa na mfululizo wa Matukio ya kihalifu na kuongeza kuwa kila aliyehusika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. “Vitendo hivi si uungwa ni Ukatili, hatutawatia hatiani Wasiohusika lakini kila aliyehusika hatutamsamehe” Alionya Dkt Shein.

Aidha Dkt. Shein amelaani kushamiri kwa Vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo ubakaji hasa kwa Watoto ambapo jumla ya Watoto wakike 480 Zanzibar wamebakwa katika kipindi cha mwezi Julai 2012 hadi Aprili mwaka huu.

Amesema hilo ni jambo la kushtua sana na kwamba wakati umefika kila mmoja kuchukua hatua zinazofaa kudhibiti hali hiyo. Dkt Shein ametoa wito kwa Wananchi na Viongozi wote kuendelea kupendana bila kuchukiana na kulinda Amani, Umoja na Kuvumiliana kwa manufaa ya Zanzibar.

Amesema panapotokea tofauti za hoja kuhusu suala la Maendeleo ya Nchi jambo la busara ni kuzungumza na kujadili kwa kuzingatia sheria zilizopo kwa manufaa ya Zanzibar. Dkt Shein ametoa Shukrani kwa Jeshi la Polisi kwa kudumisha hali ya amani katika kipindi chote cha Mwezi wa Ramadhani na kulitaka Jeshi hilo lizidishe juhudi zake kipindi cha Sherehe za Idd na siku za usoni.

Kabla ya Baraza la Idd Dkt Shein alitoa Mkono wa Idd kwa Wazee na Watu wasiojiweza katika hafla iliyofanyika Ikulu mjini Zanzibar.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

Post a Comment

أحدث أقدم