Alipotoka
kwenye jumba la Big Brother Africa, mwakilishi wa Ghana, Selly mwezi
uliopita aliahidi kumchukulia hatua za kisheria Ammy Nando kwa kusambaza
habari ya uongo kumhusu.
Wiki mbili baada ya Nando kuondolewa kwenye shindano hilo, Selly amebadilisha mawazo yake.
Kwenye mahojiano ya na gazeti linalouza zaidi nchini Ghana, Graphic Ghana,Selly amesema hana mpango wa kumshtaki tena Nando kwakuwa Mungu ameingilia kati na kumpigania.
“Hapana, sitachukua hatua zozote za kisheria dhidi ya Nando sababu
Mungu amejibu sala zangu na ameniokoa. Ameipigania vita yangu, na leo
Afrika nzima imekuja kufahamu Nando ni mtu wa aina gani na hiyo ni
hukumu tosha kwangu.
Tangu nimereja, nimekuwa nikimuomba Mungu kuingilia kati na kurudisha heshima yangu lakini kwa njia yake mwenyewe Mungu, amenionesha mimi ni mwenye haki.
Tangu nimereja, nimekuwa nikimuomba Mungu kuingilia kati na kurudisha heshima yangu lakini kwa njia yake mwenyewe Mungu, amenionesha mimi ni mwenye haki.
Hata kabla Nando hajatolewa, niliambiwa na waandaji wa Big Brother
nisichukue hatua yoyote ya kisheria dhidi yake na nilijiuliza ni vipi
nitasafisha jina langu na kurekebisha heshima yangu iliyoharibiwa lakini
Mungu alikuwa na mipango yake kwangu. Huo ulikuwa ni mchezo wa Nando
kuniondoa kama mshindani mwenye nguvu lakini Mungu anayejua zaidi
hakuniweka kwenye aibu,”alisema Selly.
Selly amesema ingawa hajasikia chochote kutoka kwa Nando baada ya
kuondolewa, hakuwa tayari kukubali ombi lake la msamaha kama angemuomba.
“Sitamsamehe kamwe Nando kwa si tu kunidhalilisha mimi na familia
yangu, nchi yangu na mpenzi wangu aliyeumizwa na maneno na fedheha muda
wote huo. Ameniletea madhara makubwa kwenye heshima yangu na kile
alichokifanya hakistahimiliki,”alisema.
“Kinachoumiza zaidi ni kwamba, sikuwa na fursa ya kujitetea mwenyewe
humo kwasababu sikusikia chochote kile hadi pale nilipotoka na
niliumizwa zaidi kwasababu sikujua jinsi mpenzi wangu alivyojisikia,
niliporudi nyumbani nashukuru amekuwa nguzo imara nyuma yangu.”
Kwa sasa, Selly, ambaye jina lake halisi ni Selorm Galley yupo chini
ya usimamizi wa kampuni ya ARV Media na yupo tayari kuingia tena kwenye
uigizaji wa filamu
إرسال تعليق