TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Baraza la
Wawakilishi la Zanzibar, lililokutana hivi karibuni na kukamilisha
Mkutano wake wa Kumi na Mbili kwa umakini mkubwa, limeashiria kuwa ni
chombo muhimu cha wananchi na pia moja ya mihimili mikuu imara ya dola
katika kusimamia na kutekeleza majukumu yake kwa maslahi ya Nchi.
Heko Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, wa pande zote, kwa
namna walivyosimama kuwasilisha michango yao, kujenga hoja, na hata
ilipobidi kuihoji na kuibana Serikali pale ilipostahili, kwa kuzingatia
maslahi ya maendeleo na ya wananchi waliowachagua.
Pongezi kwa Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, Naibu Spika,
Wenyeviti wa Baraza, Viongozi na Wajumbe wa Kamati na Daraja mbali mbali
kutokana na hikma na busara zilizoonyesha dira ya matumaini ambapo Nchi
inahitaji kuelekea, umma umewashuhudia.
Chama cha Wananchi, CUF, kinachukulia ujasiri huo wa hali ya juu wa
wahusika wote wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, kuwa ni ushindi wa
jumla wa Wazanzibari.
Zanzibar ni Nchi inayohitaji mafanikio ya maendeleo katika ngazi
zote, kupitia misingi muhimu ya demokrasia na utawala bora, chini ya
Serikali ya Umoja wa Kitaifa, ambayo sasa imeweza kuangaza matumaini ya
kweli ya ukombozi wa Wazanzibari wote.
Zama za ubabaishaji, ubadhirifu, ufisadi wa kupindukia, ubaguzi,
vitisho na kila aina ya hujuma dhidi ya wananchi, Wawakilishi wa
wananchi, watendaji waaminifu na waadilifu, na watetezi wote wa mali ya
umma, zimepitwa na wakati duniani kote; huu ni wakati wa kuishi kwa
kuchunga haki, demokrasia, utawala bora, sheria, umakini, na uwazi
usioleta shaka.
Wajumbe wote wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar wanayo haki, bila
ya vitisho, ya kuhoji, kulaumu, kukemea na hata kukataza inavyostahiki,
kila aina ya uovu na ubadhirifu hasa ule ambao Serikali inaendelea
kuufumbia macho, na hayo ndiyo matarajio na maslahi ya umma.
Wazanzibari walishuhudia na kujenga matumaini, kupitia Mkutano huo wa
Baraza la Wawakilishi, juu ya Miswada Miwili ya Sheria iliyopitishwa:
Mswada wa Sheria ya Kutoza Kodi na Kubadilisha baadhi ya Sheria za Fedha
na Kodi kuhusiana na Ukusanyaji na Udhibiti wa Mapato ya Serikali na
Mambo mengine yanayohusiana na hayo, na pia Mswada wa Sheria ya Matumizi
ya Fedha za Umma (Appripriation Bill).
Matumaini hayo yanakuja juu ya ile hima ya kudhibiti mianya ya
uvujaji na ukusanyaji wa mapato ya Serikali, kupitia utaratibu bora, na
hilo ndilo ambalo Wawakilishi wao wenye azma njema wamekuwa wakilipigia
kelele mara kwa mara.
La kushangaza na la kujiuliza ni mara ngapi Kamati za Baraza la
Wawakilishi wamewasilisha ushahidi wa kutosha wa kitaalamu juu ya
ubadhirifu na ufisadi unaotendwa na baadhi ya Watendaji wasiokuwa
waaminifu na hadi sasa hazijaonekana hatua za kinidhamu? Nini watarajie
wananchi juu ya mwenendo huo wa baadhi ya Watendaji wa Serikali, kama
siyo kuendelea kufichua maovu, hata ambayo ni siri, ambayo mamlaka bado
zinaendelea kuyakumbatia?
Kwa hili, Chama cha Wananchi, CUF, kinasema Wawakilishi lazima
waendelee kuwa wakali bila woga, wasiogope vitisho, kwani wanaoteseka na
kuteketea zaidi ni umma wa wananchi ambao ndio walipakodi.
Kuhusiana na vikundi na hata vyama vinavyojaribu kutafuta takwimu za
wananchi kwa hiari, lazima ieleweke kwamba Jumuiya, Taasisi na Asasi za
Kiraia, zinawajibika Kisheria na Kikatiba kufuatilia katika jamii ili
kuelewa na kujiridhisha, nani anafuatilia nini na anawakilishwa vipi
katika Mamlaka za Uwakilishi na hata katika kuongoza Nchi, hivyo hakuna
mantiki yoyote ya vitisho, ghilba, au maonyo kutoka kwa viongozi.
Lazima ikumbukwe kwamba lipo Agizo la Msajili wa Vyama vya Siasa la
kuzitaka jumuiya na taasisi husika kuratibu, kuhakiki, na kukuza taarifa
za Wanachama kila inapowezekana ili kujenga ufanisi; hili si ajabu
kwani Masheha wote, kwa muda mrefu, wamekuwa wakiendesha zoezi hilo, na
kwa kukitumikia Chama fulani, hivi sasa CUF imo katika shughuli muhimu
ya kukusanya Taarifa za wanachama wake katika majimbo yote, huu ni
wajibu wetu kama Chama na Taasisi halali iliyosajiliwa nchini. “CUF
haifanyi sense kama ilivyofikiriwa na ni vyema vyombo vya Ulinzi na
Usalama, wakuu wa Mikoana, wilaya na Masheha walitambue hili na kuacha
jazba ya kutaka kuvunja zoezi hetu hili ambali kwa Chama chetu ni muhimu
sana.
Msajili alipoziona ofisi yetu ya Makao Makuu hivi karibuni alitutaka
na kutuhimiza kuwatambuwa wanachama wetu kila tawi, Jimbo na wilaya na
kuweka kumbu kumbu zao vizuri. CUF haingependa kuingiliwa katika shuguli
na wajibu wake na kwa mujinu wa sheria.
Chama cha Wananchi, CUF, kinaitaka Serikali kuonya na kuwaadhibu, kwa
mujibu wa Sheria, watu wanaowafanyia hila au vurugu wananchi wenzao
wasijiandikishe katika Daftari la Kudumu la Wapigakura, almuradi
wanafuata utaratibu halali; hilo ni kosa la jinai na ni vyema
atakayebainika kufanya hivyo achukuliwe hatua za kisheria.
Chama cha Wananchi, CUF, kinalaani mwenendo huo na kinaitaka Serikali
kuwa makini hasa wakati huu ambao wananchi wanashuhudia ubadhirifu
mkubwa wa zoezi hilo, ambapo yanaonekana makundi kwa makundi ya watoto
na watu wasiostahiki, wakipelekwa kwa magari, kwenda katika Ofisi za
Wilaya, wakiandikishwa, kinyume na utaratibu, huku watu ambao
wanastahiki, wakinyimwa haki yao hiyo.
Kinachosikitisha zaidi wakati huu ambao Viongozi Wakuu wa Serikali,
usoni mwa malka za kutunga na kusimamia Sheria, wakisisitiza umuhimu wa
amani, utulivu na mshikamano, ambayo hayapatikani pasi na kuzingatia
haki, umma unashuhudia, kwa makusudi wananchi wakinyimwa nafasi yao hiyo
ya kisheria.
HAKI SAWA KWA WOTE
…………………………….
Post a Comment