Tahadhari ya Wizara ya Maji juu ya utapeli wa kutumia simu, vyeo, majina ya viongozi

 
TAARIFA KWA UMMA
Kwa wiki kadhaa sasa, kumejitokeza wimbi la vitendo vya kitapeli la kutuma ujumbe mfupi wa maneno (SMS) pamoja na kupiga simu kwa baadhi ya Wakurugenzi Watendaji wa Mamlaka za Majisafi na Majitaka Mijini katika Mikoa mbalimbali wakijitambulisha wao ni Mhe Waziri wa Maji au Mhe. Naibu Waziri wa Maji na kuwa wanahitaji msaada wa fedha au wao wametumwa na vingozi hao.

Wizara ya Maji inapenda kuutaarifu Umma kuwa, watu hao ni matapeli na tunasisitiza kuwa shughuli zote zinazofanywa na viongozi wa Wizara hugharamiwa na Wizara yenyewe kulingana na mpango wa 
bajeti husika. Hivyo, sio kweli kuwa Mhe.Waziri au Mhe.Naibu Waziri wa Maji anaweza kupiga simu kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Malaka ya Maji safi na Majitaka kuomba msaada.

Wizara ya Maji inasisitiza kuwa, Wakurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka wote Mijini ni marufuku kufanya malipo yoyote yasiyofuata maelekezo na taratibu za sheria za fedha na watu wasiowafahamu kwa kisingizio cha kutumwa na viongozi. Lengo la matapeli hao ni kujipatia fedha na njia zisizo halali kwa kuchafua majina ya Mawaziri wa Wizara yetu. 

Kitendo cha kutuma SMS za kughushi au kupiga simu na kuiga sauti za viongozi wa Wizara ni kosa la jinai na tunaomba ushirikiano toka kwa wananchi wote pamoja na vyombo vya dola ili kukabiliana na utapeli huu mpya ulioanza kujichomoza.

Imetolewa na,

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

WIZARA YA MAJI

Post a Comment

Previous Post Next Post