TANGAZO UZINDUZI WA MPANGO WA KULETA MATOKEO MAKUBWA SASA (BIG RESULTS NOW) KATIKA SEKTA YA ELIMU


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa (MB), anawaalika wadau wote wa Elimu nchini kwenye Maonesho ya Wazi ya Uzinduzi wa Mpango wa Kuleta Matokeo Makubwa Sasa (Big Results Now – BRN) katika Sekta ya Elimu Tanzania.

Maonesho haya yatafanyika siku ya Alhamisi tarehe 15/08/2013 kuanzia saa tatu (3.00) Asubuhi kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere uliopo karibu na viwanja vya Gymkana.

Lengo kuu ni kuelimisha na kupata maoni ya Wadau katika utekelezaji wa vipaumbele vya Sekta ya Elimu ili kuleta Matokeo Makubwa Sasa. Wananchi wote mnakaribishwa, hakuna kiingilio.

“Tuwajibike, Tujitume Sasa kwa Maendeleo Makubwa ya Elimu Tanzania”

Tangazo hili limetolewa na:
Katibu Mkuu,
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

Post a Comment

أحدث أقدم