VIFO vya samaki katika ziwa Nyasa katika Wilaya ya Nyasa
mkoani Ruvuma, vimezusha hofu kati ya Tanzania na Malawi kutokana na kila
upande kuhisi umetupa fataki ziwani humo. Hisia hizo zinatokana na pande mbili
hizo kuwa kwenye mgogoro wa mpaka.
Kauli
hiyo ilitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira),
Dkt.Teresa Huvisa, akizungumza na wananchi kandoni mwa Ziwa Nyasa wakati wa
ziara yake ya siku tatu mkoani Ruvuma, alisema;“Nimepata taarifa kuwa samaki
wanaokufa katika Ziwa Nyasa sasa wameleta hofu kwa wananchi wa nchi zote mbili
Tanzania na Malawi, kwa hiyo ninachoweza kuwaambia ni kwamba tutatuma wataalamu
kuchunguza chanzo cha samaki kufa,” alisema Dkt. Huvisa.
Lakini pia kuna wavuvi wanatumia
majani yanayoitwa mtunungu kuvulia samaki ambayo ukimwaga ziwani au mtoni
samaki wanakufa, kwa hiyo msitumie sumu kuvulia samaki.
Alisema samaki hao wanakufa ziwani
humo bila kujua chanzo chake msiwale.
Hata hivyo aliwatoa hofu wananchi
hao waishio mpakani mwa nchi ya Malawi na Msumbiji kutokana na mzozo wa
kugombea umiliki na mpaka wa ziwa hilo kati ya Tanzania na Malawi, kutoogopa
mzozo huo na kwamba Malawi haina ubavu wa kupigana na Tanzania endapo nchi hizo
zitaingia vitani
إرسال تعليق