Kadhi
Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis(mwenye koti jeusi) na
Mwenyekiti wa Vodacom Foundation Hassan Saleh (kulia) wakiwa katika
picha ya pamoja na wafanyakazi wa Vodacom na baadhi ya wanafunzi wa
Madrasa za Kisiwani Pemba mara baada ya zoezi la kukabidhi sadaka ya
vyakula na vifaa vya shule kwa wanafunzi hao muda mfupi kabla ya wote
kushiriki futrari iliyoandaliwa na Vodacom Foundation kwenye uwanja wa
Gombani Kisiwani Pemba mwishoni mwa wiki.
Mfanyakazi
wa Vodacom Tanzania Jaffary Juma akikabidhi vyakula vilivyotolewa na
Vodacom Foundation kwa wanafunzi wa madrasa mbalimbali za Kisiwani Pemba
tukio lililohusisha pia futari kwa ajili ya wanafunzi hao na wadau wa
Vodacom Kisiwani humo iliyofanyika uwanja wa Gombani mwishoni mwa wiki.
Wanaoshuhudia ni Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis(mwenye
koti jeusi) na Mwenyekiti wa Vodacom Foundation Hassan Saleh (kulia) na
wafanyakazi wa Vodacom.
Meneja Uhusiano wa Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim akizungumzia kampeni ya Pamoja na Vodacom namna
inavyotekelezwa wakati wa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa
kuandaa futari na kutoa sadaka ya vyakula na vifaa vya shule kwa
wanafunzi wa madrasa sehemu mbalimbali nchini. Mwaka huu Vodacom
Foundation ilitenga Sh. 50 Milioni kwa ajili ya kampeni hiyo na
kuwafikia wanafunzi zaidi ya 2500.
Kadhi
Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis akisalimiana na viongozi
mbalimbali wa dini ya kiislamu wakati akiwasili kwenye ukumbi wa Uwanja
wa Gombani Pemba tayari kuongoza hafla ya kufuturisha iliyoandaliwa na
Vodacom Foundation mwishoni mwa wiki kwa ajili ya wanafunzi wa Madrasa
na wadau wa kampuni hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Vodacom Foundation
Hassan Saleh
إرسال تعليق