Wakala wa Majengo (TBA), ulianzishwa mwaka 2002
kupitia Sheria ya Wakala Namba 30 ya mwaka 1997. Lengo la kuanzishwa TBA ni
kutoa huduma bora na ya gharama nafuu ya makazi kwa watumishi wa umma na ofisi
kwa Serikali na Taasisi zake.
Ikiwa ni taasisi muhumu ya Serikali iliyochini
ya Wizara ya Ujenzi, TBA imeshiriki maonesho ya Wakulima maarufu Nane Nane
ambayo hii leo yanafikia Kilele katika kanda mbalimbali na Kitaifa yanafikia
Kilele katika Viwanja vya Nzuguni, mjini Dodoma.
Timu ya TBA iliyo katika banda lao Viwanja vya
Nzuguni jana ilitembelewa na Blog hii na kuikuta ikiwa kamili katika utoaji
huduma kwa wananchi ya nini ambacho TBA inakifanya kila siku katika utekelezaji
wa shughuli zake.
Timu hiyo pichani kutoka kushoto ni Kaimu Afisa
Uhusiano, Mariam Lusewa, Meneja Miradi Maalum, Edwin Nnunduma, Afisa Miliki, Pendaeli
Mhufu na Mhandizi Mazingira, Mtapuli Juma.
Afisa Miliki, Pendaeli Mhufu (kushoto) akihudumia wananchi.
Wageni wakisaini kitabu cha kutembelea banda hilo na kutoa maoni yao juu ya huduma.
Kutoka
Kulia ni Pendaeli Mhufu, Mariam Lusewa na Mtapuli Juma wakiwa na nyuso
za furaha wakati wa kuhudumia wananchi waliotembelea banda lao Nzuguni
Dodoma.
Kaimu
Afisa Uhusiano, Mariam Lusewa akiwasikiliza mwananchi aliyetembelea banda lao
jana kupata taarifa mbalimbali.
Meneja
Miradi Maalum, Edwin Nnunduma pamoja na Kaimu Afisa Uhusiano, Mariamu
Lusewa wakiwasikiliza wananchi na kuwapa maelezo ama majibu ya maswali
yao.
Kaimu
Afisa Uhusiano, Mariam Lusewa akimsikiliza mwananchi aliyetembelea banda lao
jana kupata taarifa mbalimbali.
إرسال تعليق