Kikosi cha Young Africans kilichoanza leo dhidi ya 3 Pillars
Young Africans imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya timu ya 3 Pillars
FC kutoka Lagos Nigeria katika mchezo wa kirafiki uliofanyika leo jioni
katika dimba la uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara Young Africans waliingia uwanjani kwa
lengo la kusaka ushindi na kuendeleza rekodi ya ushindi katika michezo
ya kirafiki ya kujipima nguvu inayocheza kwa ajili ya maandalizi ya
msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom 2013/2014.
Ikiwa tumia washambuliaji wake wapya Hussein Javu na Mrisho Ngassa
waliojiunga na kikosi msimu huu, Yanga ilikosa nafasi za wazi za
kufungua kupitia kwa washambuliaji hao ambao hawakuonekana kuwa makini
makini katika umaliziaji wa mipira iliyokuwa ikiwafikia.
David Luhende alikosa bao dakika ya 34 kufuatia mpira alioupiga
kuokelewa na mlinda mlango wa 3Pillars FC na kuwa kona ambayo haikuzaa
matunda, huku awali Said Bahanuzi akikosa nafasi pia kama hiyo dakika ya
17 ya mchezo.
Hussein Javu aliipatia Young Africans bao kwanza dakika ya 40 ya mchezo
kwa ustadi akiitumia vizuri nafasi hiyo aliyopewa na kuingo Athuman Idd
'Chuji' aliyewazidi ujanja walinzi wa 3Pillars FC na kumpasia Javu
aliyeukwamisha mpira wavuni na kuhesabu bao kwa watoto wa Jangwani.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans -0 3Pillars FC.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ambapo Yanga
iliwaingiza Didier Kavumbagu, Kelvin Yondani, Oscar Joshua, na Salum
Telela kuchukua nafasi za Nadir Haroub, Jerson Tegete, Juma Abdul na
Said Bahanuzi mabadiliko ambayo yaliongeza kasi ya mchezo.
David Luhende ambaye leo alikuwa mwiba kwa timu ya 3Pillars FC nusura
aipatie Yanga bao la pili lakini mpira alioupiga ulikokolewa na walinzi
wa timu hiyo ya Nigeria na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.
Yanga iliendelea kulishambulia lango la 3Pillars dakika zote za mchezo
lakini kutokua makini kwa mshambuliaji Didier Kavumbagu na Hussein Javu
kuliendelea kuufanya ubao wa mabao uendelee kusomeka 1-0.
Mpaka dakika 90 za mwamuzi Oden Mbaga zinamalizika, Young Africans 1-0 3Pillars FC .
Kesho kikosi cha Yanga hakitakua na mazoezi na wachezaji wote watakua na
mapumziko kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Eid na waterejea tena
mazoezini siku ya jumamosi asubuhi katika uwanja wa Loyola kuendelea
kujifua na maandalizi ya Ligi Kuu.
Young Africans: 1.Ally Mustapha 'Barthez', 2.Juma Abdul/Salum Telela,
3.David Luhende, 4.Nadir Haroub 'Cannavaro'/Kelvin Yondani, 5.Rajab
Zahir, 6.Athuman Idd 'Chuji/Issa Ngao, 7.Said Bahanuzi/Abdallah Mguhi
'Messi'/Shaban Kondo, 8.Haruna Niyonzima/Bakari Masoud, 9.Jerson
Tegete/Didier kavumbagu, 10.Hussein Javu, 11.Mrisho Ngassa
إرسال تعليق