MAELEZO YA MSINGI KUHUSU MTI WA MLONGE (Moringa Oleifera)~~
A/Alleykum,
Moringa (Moringa spp.) maarufu kama Mlonge ni miongoni mwa miti muhimu
kuliko yote duniani. Mti huu ukuao haraka hupandwa katika maeneo mengi
na hutumika kama chakula cha binadamu, lishe ya mifugo, tiba mbadala na
kusafisha maji.
Faida na matumizi ya mti wa Moringa:
1. Virutubishi
Faida na matumizi ya mti wa Moringa
Karibu kila sehemu ya mti wa Moringa inatumika au inalika kama chakula.
Majani ndio sehemu kuu ya mti wa Moringa, unaweza kuyala yakiwa mabichi
au yakiwa yamepikwa kama mboga yoyote ya majani, na pia unaweza
ukayakausha na kuyahifadhi kama unga-unga kwa miezi mingi huku ukitumia
kama kiungo kwenye mboga na mchuzi. Pia majani yanaweza kutumika kama
lishe bora ya mifugo.
Utafiti wa kisayansi umeonyesha kuwa majani ya
Moringa ni chanzo kikubwa cha virutubishi vingi sana. Virutubishi hivi
ni pamoja na;
Vitamini C - Kirutubishi hiki ni muhimu katika
kutengeneza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali. Kiwango chake
katika majani ya Moringa ni zaidi ya mara saba ya ile inayopatikana
kutoka kwenye machungwa.
Calcium (madini chuma)- Kirutubishi hiki ni
muhimu katika kuimarisha pamoja na kujenga mifupa na meno mwilini.
Kiwango chake katika majani ya Moringa ni mara nne zaidi ya yale
yanayopatikana kutoka kwenye maziwa.
Protini- Kirutubishi hiki ni
muhimu katika kujenga mwili na kuimarisha ngozi. Kiwango chake katika
majani ya Moringa ni mara mbili zaidi ya ile inayopatikana kutoka kwenye
maziwa.
Vitamini A- Kirutubishi hiki ni muhimu katika kuimarisha
macho na kuongeza uwezo wa kuona. Kiwango chake katika majani ya Moringa
ni mara nne zaidi ya ile inayopatikana kutoka kwenye Karoti.
Potassium- Kirutubishi hiki ni muhimu katika kujenga na kuupatia mwili
nguvu. Kiwango chake katika majani ya Moringa ni mara tatu zaidi ya ile
ipatikanayo kutoka kwenye ndizi.
Maua ya Moringa yamejaliwa madini
chuma (calcium) na Potassium kwa wingi na yanaweza kuchemshwa au kupikwa
na kuliwa kama mboga.
2. Mboga
Majani ya Moringa huliwa kama
mboga nyingine za majani kwa mfano mchicha. Majani yanaweza kuvunwa
wakati wa kiangazi ambapo mboga nyingine hazipatikani.
Pia matunda mateke ya Moringa huweza kutumika kama mboga, hutayariswa kama maharage mabichi (machanga).
Matunda yalikomaa hutoa mbegu ambazo zinaweza kutumika kama njegere au kukaangwa kama karanga.
3. Mafuta
Mafuta kutoka kwenye mbegu za mti wa Moringa huweza kutumika katika
kupikia na kuwasha katika nyumba. Pia hutumika sana kwenye viwanda
katika utengenazaji wa sabuni na bidhaa za urembo. Mafuta hukamuliwa
kutoka kwenye mbegu kama ambavyo alizeti hukamuliwa.
Tiba mbadala:
Moringa ni mti muhimu sana katika utabibu kama tiba mbadala, majani,
maua, mbegu na mizizi yake hutumika sana katika kutibu magonjwa
mbalimbali.
Majani
• Majani mabichi ya Moringa ni mazuri kwa
kina mama wajawazito na wenye kunyonyesha, huongeza wingi wa maziwa na
hushauriwa kwa kutibu Anaemia.
• Juisi ya majani ya Moringa hutumika
kusafisha tumbo na hutibu magonjwa ya zinaa. Juisi ikichanganywa na
asali inatibu kuharisha.
• Pia juisi ina uwezo wa kusawazisha presha (BP) na kudhibiti viwango vya sukari kwa wagonjwa wenye kisukari.
• Majani pia huweza kupakwa mwilini katika kutibu majipu na maambukizi ya ngozi.
Mbegu
• Mbegu za mti wa Moringa ni kinga dhidi ya vijidudu (bacteria) wasababishao magonjwa na kuathiri ngozi.
• Pia mbegu hutuminka katika kusafisha au kuchuja maji ambapo
zikipondwa na kuwekwa kwenye maji yenye tope au machafu husababisha
uchafu kujikusanya na kuzama chini kisha kuacha maji yakiwa safi na
salama kwa kupikia au kunywa baada ya kuchemsha.
Magome
•
Magome ya mti wa Moringa hupondwa na kuwa rojorojo kisha hutumika kutibu
majipu pia hupakwa ili kupunguza maumivu yatokanayo na kung’atwa na
wadudu kama nyoka na nge.
Matumizi mengineyo
Miti ya Moringa
ikipandwa shambani huweza kuwa msaada kwa mimea ipandayo kama vile
maharage. Pia Moringa ikipandwa bustanini husaidia kupunguza joto la
moja kwa moja kufikia mimea kama vile mboga mboga na kupunguza uwezekano
wa mboga kusinyaa au kukauka.
..............Ama kwa hakika Allaah subhannahu wa Ta'ala ametupa NEEMA KUBWA:
A/Alleykum,
Moringa (Moringa spp.) maarufu kama Mlonge ni miongoni mwa miti muhimu kuliko yote duniani. Mti huu ukuao haraka hupandwa katika maeneo mengi na hutumika kama chakula cha binadamu, lishe ya mifugo, tiba mbadala na kusafisha maji.
Faida na matumizi ya mti wa Moringa:
1. Virutubishi
Faida na matumizi ya mti wa Moringa
Karibu kila sehemu ya mti wa Moringa inatumika au inalika kama chakula. Majani ndio sehemu kuu ya mti wa Moringa, unaweza kuyala yakiwa mabichi au yakiwa yamepikwa kama mboga yoyote ya majani, na pia unaweza ukayakausha na kuyahifadhi kama unga-unga kwa miezi mingi huku ukitumia kama kiungo kwenye mboga na mchuzi. Pia majani yanaweza kutumika kama lishe bora ya mifugo.
Utafiti wa kisayansi umeonyesha kuwa majani ya Moringa ni chanzo kikubwa cha virutubishi vingi sana. Virutubishi hivi ni pamoja na;
Vitamini C - Kirutubishi hiki ni muhimu katika kutengeneza kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali. Kiwango chake katika majani ya Moringa ni zaidi ya mara saba ya ile inayopatikana kutoka kwenye machungwa.
Calcium (madini chuma)- Kirutubishi hiki ni muhimu katika kuimarisha pamoja na kujenga mifupa na meno mwilini. Kiwango chake katika majani ya Moringa ni mara nne zaidi ya yale yanayopatikana kutoka kwenye maziwa.
Protini- Kirutubishi hiki ni muhimu katika kujenga mwili na kuimarisha ngozi. Kiwango chake katika majani ya Moringa ni mara mbili zaidi ya ile inayopatikana kutoka kwenye maziwa.
Vitamini A- Kirutubishi hiki ni muhimu katika kuimarisha macho na kuongeza uwezo wa kuona. Kiwango chake katika majani ya Moringa ni mara nne zaidi ya ile inayopatikana kutoka kwenye Karoti.
Potassium- Kirutubishi hiki ni muhimu katika kujenga na kuupatia mwili nguvu. Kiwango chake katika majani ya Moringa ni mara tatu zaidi ya ile ipatikanayo kutoka kwenye ndizi.
Maua ya Moringa yamejaliwa madini chuma (calcium) na Potassium kwa wingi na yanaweza kuchemshwa au kupikwa na kuliwa kama mboga.
2. Mboga
Majani ya Moringa huliwa kama mboga nyingine za majani kwa mfano mchicha. Majani yanaweza kuvunwa wakati wa kiangazi ambapo mboga nyingine hazipatikani.
Pia matunda mateke ya Moringa huweza kutumika kama mboga, hutayariswa kama maharage mabichi (machanga).
Matunda yalikomaa hutoa mbegu ambazo zinaweza kutumika kama njegere au kukaangwa kama karanga.
3. Mafuta
Mafuta kutoka kwenye mbegu za mti wa Moringa huweza kutumika katika kupikia na kuwasha katika nyumba. Pia hutumika sana kwenye viwanda katika utengenazaji wa sabuni na bidhaa za urembo. Mafuta hukamuliwa kutoka kwenye mbegu kama ambavyo alizeti hukamuliwa.
Tiba mbadala:
Moringa ni mti muhimu sana katika utabibu kama tiba mbadala, majani, maua, mbegu na mizizi yake hutumika sana katika kutibu magonjwa mbalimbali.
Majani
• Majani mabichi ya Moringa ni mazuri kwa kina mama wajawazito na wenye kunyonyesha, huongeza wingi wa maziwa na hushauriwa kwa kutibu Anaemia.
• Juisi ya majani ya Moringa hutumika kusafisha tumbo na hutibu magonjwa ya zinaa. Juisi ikichanganywa na asali inatibu kuharisha.
• Pia juisi ina uwezo wa kusawazisha presha (BP) na kudhibiti viwango vya sukari kwa wagonjwa wenye kisukari.
• Majani pia huweza kupakwa mwilini katika kutibu majipu na maambukizi ya ngozi.
Mbegu
• Mbegu za mti wa Moringa ni kinga dhidi ya vijidudu (bacteria) wasababishao magonjwa na kuathiri ngozi.
• Pia mbegu hutuminka katika kusafisha au kuchuja maji ambapo zikipondwa na kuwekwa kwenye maji yenye tope au machafu husababisha uchafu kujikusanya na kuzama chini kisha kuacha maji yakiwa safi na salama kwa kupikia au kunywa baada ya kuchemsha.
Magome
• Magome ya mti wa Moringa hupondwa na kuwa rojorojo kisha hutumika kutibu majipu pia hupakwa ili kupunguza maumivu yatokanayo na kung’atwa na wadudu kama nyoka na nge.
Matumizi mengineyo
Miti ya Moringa ikipandwa shambani huweza kuwa msaada kwa mimea ipandayo kama vile maharage. Pia Moringa ikipandwa bustanini husaidia kupunguza joto la moja kwa moja kufikia mimea kama vile mboga mboga na kupunguza uwezekano wa mboga kusinyaa au kukauka.
..............Ama kwa hakika Allaah subhannahu wa Ta'ala ametupa NEEMA KUBWA:
إرسال تعليق