Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa pamoja na diwani wa TLP
Ntabo Majabi kata ya MwendaKulima wakati wa uzinduzi wa jengo la kituo
cha afya kilichodhaminiwa na mgodi wa Buzwagi kulia ni Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
DIWANI wa
Kata Mwendakulima Ntabo Majabi kupitiaTanzania Labour Party (TLP), amesema Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrhaman Kinana ni kiongozi mwenye busara na hekima kubwa na
ndio maana Rais Jakaya Kikwete amemua kumpa nafasi hiyo kwa kuwa atakuwa
anamjua vizuri.
Akizungumza
katika uzinduzi wa kituo cha afya katika eneo hilo, alisema amefurahishwa na
aina ya siasa ambazo zinafanywa na Kinana na yeye binafsi ametambua kuwa Katibu
Mkuu huyo wa CCM anaouwezo mkubwa wa kufanya kazi zake.
“Kinana wewe
ni jembe, wakati unazungumza nilikuwa nimekaa mbali na kusikiliza lakini
maelezo yako yamenifurahisha na ndio maana nimeamua kuja kukupa mkono.Kama nchi
hii ingekuwa na makatibu wakuu wengi wa aina yako, tungepiga hatua hasa katika
siasa za nchi hii.
“Pia
niwaambie wananchi siasa si ugomvi, Kinana ameeleza vizuri, tunatakiwa
kushirikiana ili kufanikisha malengo ya kuwatumikia wananchi.Nakupongeza mzee
Kinana kwa maelezo yako yamenipa faraja licha ya kwamba mimi ni diwani kupitia
TLP,”alisema.
Ndugu Kinana
alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha wananchi kuwa CCM ndio yenye Serikali na
diwani huyo licha ya kuwa TLP bado anatekeleza ilani ya CCM , hivyo wananchi
nao wanatakiwa kutambua hakuna sababu ya kulumbana kwasababu tu ya mambo ya
siasa.
Post a Comment