Naibu rais wa Kenya William Ruto
pamoja na mshukiwa mwenzake Joshua Arap Sang wamesomewa mashtaka
yanayowakabili katika mahakama ya kimataifa ya ICC
12:01 Upande wa mashtaka unasimulia ambavyo
unapanga kuthibitisha kuwa kesi yao ni ya uhakika, ushahidi utakaotolewa
, na nani atakayetoa ushahidi huo. Mashahidi inasemekana watawataja
wahusika wengine kwenye kesi hiyo hasa walioshirkiana na washtakiwa
kuendesha 11:51 Bensouda aambia mahakama kuwa amekuwa na wakati mgumu sana kukusanya ushahidi wa kesi yake akisema kuwa wengi wa mashahidi wamejiondoa katika kesi hiyo wakisema wanahofia maisha yao na kuongeza kuwa baadhi pia wamehongwa ili wasitoe ushahidi wao
11:41 Fatou Bensuda mwendesha mkuu wa mashtaka katika mahakama hiyo aelezea mahakama kuhusu tuhuma zinazowakabili Ruto na Sang kwa kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi mkuu mwaka 2007-2008. Bansuda amesema kuwa Ruto alifanya mauaji kwa sababu za kisiasa huku Sang akimsaidia kuchochea ghasia ili kumsaidia kufanikisha ajenda yake ya kuingia mamlakani
11:35 Joshua Sang pia amekanusha mashtaka yote dhidi yake
11:33 Ruto amekana mashtaka yote aliyosomewa na upande wa mashtaka kuwa alihusika na uhalifu dhidi ya binadamu , mauaji, dhulma na kuwaondosha watu makwao kwa lazima
11:23 Ruto asomewa mashtaka dhidi yake na kuambiwa kuwa alihusika na mauaji ya watu katika mkoa wa Rift Valley
11:20 Kesi dhidi ya mshukiwa mkuu wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu nchini Kenya Naibu Rais William Ruto imeanza kusikilizwa katika mahakama ya kimataifa ya ICC .
11:00 Wahusika wote kwenye kesi hii kutoka upande wa naibu rais Ruto, mshukiwa mwengine Joshua Arap Sang na upande wa mashtaka wake Fatou Bensauda walijitambulisha mahakamani kwa ombi la mmoja wa majaji kwenye jopo la majaji
- bbc
Post a Comment