
Timu
ya KMKM ya Kisiwani Pemba ikifurahia ushindi wake wa Ngao ya Jamii,mara
baara ya kuifunga timu ya Chuoni mabao 5-4 yaliyopatikana kwa mikwaju ya
penati baada ya kumaliza dakika tisini ya mchezo kwa kufunguma bao
1-1.Mchezo huo ulipigwa jana usiku kwenye Uwanja wa Gombani,Pemba ikiwa
ni sehemu ya ufunguzi wa Ligi kuu ya Grand Malt,Zanzibar.

Mgeni
Rasmi katika Mchezo huo wa ufunguzi wa Ligi Kuu ya Grand Malt Zanzibar
na kuwaniwa kwa Ngao ya Jamii,Waziri wa Serikali ya Mapinduzi asiekuwa
na Wizara Maalum,Mh. Haji Faki Shaali (wa pili kushoto) akikabidhi Ngao
ya Jamii kwa Nahodha wa timu ya KMKM,Ame Hamis Kibobeo mara baada ya
kutwaa Ngao hiyo kwa kufunga timu ya Chuoni kwa mikwaju ya penati
5-4,katika mchezo uliochezwa jana usiku kwenye Uwanja wa Gombani,Pemba.

Wachezaji wa KMKM wakipeana mkono na viongozi mbali mbali walikuwepo Uwanjani hapo.

Kikosi cha Timu ya Chuoni FC

Kikosi cha Timu ya KMKM.

Beki wa Timu ya Chuoni akijaribu kutaka kuondosha hatari iliyokuwa ikielekea langoni kwake.

Mshambuliaji
wa Timu ya KMKM,Juma Mbwana (8) akijaribu kutaka kumtoka Beki wa Timu
ya Chuoni,Mwinyi Haji wakati wa Mchezo wao wa kuwania Ngao ya
Jamii,uliochezwa jana Usiku kwenye Uwanja wa Gombani,Pemba.hadi mwisho
wa mchezo timu ya KMKM ilishinda kwa mabao 5-4 yaliyopatikana kwa
mikwaju ya penati.

Mchezaji wa timu ya KMKM akiondoka na mpira.

Hatari langoni mwa timu ya Chuoni.

Goooooo........hii ndio penati ya mwisho ya timu ya KMKM iliyowapatia Ushindi na mpaka kunyakua Ngao ya Jamii.

Meneja Masoko wa Kinywaji cha Grand Malt,Fimbo Butallah (kushoto) akizungumza machache kabla ya kuanza kwa mechi hiyo.

Makamu
wa Rais wa ZFA (Pemba),Ali Mohamed (kulia) akieleza jambo mbele ya
Mgeni Rasmi na viongozi wengine waliokuwepo uwanjani hapo kabla ya
kuanza kwa mchezo kati ya KMKM na Chuoni,uliochezwa jana usiku kwenye
Uwanja wa Gombani,Pemba.
إرسال تعليق