Ndege ya Serekali ya Oman iliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, iliomchukuwa Waziri wa Habari wa Oman Dkt. Abdulmonam Al Hasani, na maofisa wa Wizara hiyo kuhudhuria Kongamano la Kimataifa la Historia ya Ustaarabu wa Kiislam,Litakalofanyika kesho katika hoteli ya kitalii ya Lagema Nungwi.
Viongozi wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar na Balozi wa Oman Tanzania
wakiwa katika uwanja wa ndege wa Zanzibar kuupokea Ujumbe wa Oman
unaoshiriki katika Kongamano hilo lilliloandaliwa kwa Ushirikiano wa
mnchi tatu Zanzibar Oman na Uturuki.
Waziri wa Habari wa Oman Dkt. Abdulmonam Al Hasani, wa kwanza kulia,
akiwasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume na
Maofisa wa Wizara yake katikati Muhannad Al Raisi na Khalifa Al
Darmaki.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Aki Juma Shamuhuna,
akimsalimia Waziri wa Habari wa Oman Dkt. Abdulmonam Al Hasani,
alipowasili uwanja wa ndege wa Zanzibar kwa ajili ya kuhudhuria
kongamano la Historia ya Ustaarabu wa Kiislam.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo, Said Ali Mbarouk,
akisalimiana na mgeni wake Waziri wa Habari wa Oman, Dkt. Abdulmonam Al
Hasani.alipowasili uwanja wa ndege wa Zanzibar kwa ajili ya kuhudhuria
Kongamano la Kimataifa la Historia ya Ustaarabu wa Kiislam.
Waziri wa Habari wa Oman Dkt. Abdul Monam Al Hasani, akiwa na wenyeki wake alipowasili Zanzibar
Mwenyekiti wa Nyaraka na Kumbukumbu wa Oman Dkt. Hamad Mohammed Al
Dhiwiyan, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Juma
Shamuhuna, Waziri wa Habari wa Oman Dkt. AbdulMonam Al Hasani na Waziri
wa Utamaduni Utalii na Michezo Zanzibar Said Ali Mbarouk, wakiwa katika
ukumbi wa VIP uwanja wa ndege wa Zanzibar baada ya kuwasili kwa Waziri
huyo kuhudhuria Kongamano kesho katika hoteli ya Lagema Nungwi.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mhe, Said Ali Mbarouk,
akizungumza na Waziri wa Habari wa Oman Dkt. AbdiulMonam Al Hasani,
alipowasili Zanzibar leo kwa ajili ya kuhudhuria Kongamano la Historia
ya Ustaarabu wa Kiislam linalotarajiwa kufunguliwa na Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein. kesho katika
hoteli ya Lagema na kuwasilishwa mada 62.
Mwenyekiti wa Nyaraka na Kumbukumbu ya Oman Dkt. Hamad Mohammed Al
Dhiwiyan, akizungumza na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar
Mhe. Ali Juma Shamuhuna.
Mwenyekiti Mwenza wa Kamati ya Maandali\ya Maandalizi ya Kongamano hilo
Nd. Abdalla Mzee, akizungumza na Waandishi wa habari kukamilika kwa
Kongamano hilo na matayarisho yote kukamilika na kuwasilishwa kwa Mada
62 naZanzibar kutowa Mada 4 zitakazowakilishwa na Jaji Mkuu Zanzibar
Omar Makungu, Mada kuhusi Mahakama ya Kadhi Zanzibar kuazishwa kwake
Zanzibar miaka hiyo.Dkt. Issa Haji Zidy , Dkt Amina Ameir Issa na
Mwalimu Amour Abdalla Khamis.
Post a Comment