Liverpool wasajili Beki Mpya - Tiago Ilori

Liverpool wamemaliza uhamisho wa beki kutoka Sporting Lisbon ,Tiago Ilori  mwenye miaka 20. Ni mchezaji wa sita kunaswa na Liverpool kwenye dirisha hili wakiwemo Kolo Toure, Iago Aspas, Luis Alberto, Simon Mignolet na Aly Cissokho.


Ilori amesema anajiskia vizuri kuwa mchezaji wa Liverpool na kucheza kwenye Premier League imekuwa ndoto yake kwa muda mrefu. Akipewa nafasi Ilori amesema Ataonyesha uwezo mkubwa uwanjani na kucheza mechi nyingi awezavyo.

Liverpool inaongoza kwenye Premier League baada yakuichapa Manchester United 1-0 jumapili iliyopita.

Post a Comment

Previous Post Next Post